Washiriki wa Kongamano la kujadili sekta ya uziduaji na
uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha na Mahmoud Ahmad)
Mahmoud
Ahmad, Arusha
Zaidi ya
washiriki 56 wanashiriki katika Kongamano la kujadili sekta ya uziduaji na
uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi katika sekta za sheria,kanuni,sera
na mikataba kwa watendaji wa sekta hiyo kutoka kwenye nchi za jumuiya ya Afrika
mashariki.
Akizungumza
na vyombo vya habari mkuu wa kitengo cha madini kanda ya kaskazini(tmg)
Mhandisi Gilay Shamika alisema kuwa kongamano hilo la siku mbili lilovuta wadau
wa sekta ya madini kutoka nchi za Kenya Uganda na wenyeji Tanzania na
kuandaliwa na taasisi ya Global Academy ya nchini Uingereza.
Shamika
alisema kuwa sekta ya madini na gesi imekuwa na changamoto mbali mbali ambazo
zinahitaji elimu na ufahamu wa hali ya juu kwenye Nyanja hiyo hivyo wanakutana
kujadiliana kwa pamoja na wenzao kuweza kupata uelewa zaidi.
Aidha
alisema kuwa wadau hao kutoka sekta za sheria,madini na fedha ndioyo wanahusika
katika kongamano hilo huku wakipata uelewa ni jinsi gani watakavyoweza kuongeza
kiwango cha uchangiaji wa pato la taifa kutokana sekta ya madini hususani
Mafuta na Gesi.
Giley
alisema kuwa sekta ya madini hususani kwenye eneo la Mafuta na gesi limekuwa na
changamoto mbali mbali hivyo ni sekta muhimu kuielewa kwa mapana hivyo wao na
taasisi hiyo wanajadili kuweza kuzinufaisha nchi za ukanda huu.
No comments:
Post a Comment