HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 29, 2026

Walimu 39 waenda India kushiriki mafunzo

Alfajiri ya Machi 29, 2026 kundi la kwanza la walimu 39 kati ya jumla ya 150 limeondoka kwa ndege ya Oman Air kuelekea New Delhi, India. Safari hii ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuimarisha elimu ya ufundi na umahiri, ikilenga kuandaa walimu wenye uwezo wa kisasa na mbinu shirikishi za ufundishaji.  

Katika kipindi cha mwezi mmoja, walimu hao watashiriki katika mafunzo ya umahiri ya ufundishaji wa masomo ya Amali katika vyuo vya Sharda na Reos 9. 


Aidha, watapata nafasi ya kushiriki mafunzo kwa vitendo katika shule za ufundi na ufundi stadi nchini India, hatua itakayowawezesha kuongeza ujuzi wa vitendo na kuimarisha mbinu za ufundishaji zinazohusiana na mahitaji ya soko la ajira.  


Hii ni hatua ya kimkakati inayothibitisha dhamira ya serikali ya kuwekeza katika rasilimali watu, kuhakikisha walimu wanakuwa chachu ya mabadiliko ya elimu na ajira kwa vijana.  






No comments:

Post a Comment

Pages