Mgombea wa Urais
TUCTA, Dismas Lyassa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kushoto ni Meneja Kampeni, Khamis Tembo na Wakili Jebra Kambole.
Vipaumbele
1. Kupigania na
kulinda haki za wafanyakazi;
Katika kipaumbele
hili lengo hasa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi yakiwamo-:
i.
Kulipwa ujira/mishahara duni isiyoendana na uhalisia wa maisha.
ii.
Ucheleweshaji wa upatikanaji wa ujira/mishahara.
iii.
Ucheleweshaji fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya/ kiwango kidogo cha
fedha za kujikimu.
iv.
Uhaba au kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya
v.
Rushwa na kuajiri kwa misingi ya kujuana kwa mfano katika Halmashauri ya
Siha, wilaya ambayo imegawanywa kutoka Hai, kuna pori kubwa la West Kilimanjaro
mlimani kabisa, hakuna maendeleo…ni suala la kawaida kuona watu wakiongea
kilugha ofisini kama lugha ya Taifa.
vi.
Wakubwa yaani mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha wafanyakazi kwa kadri
wanavyotaka wao, sivyo inavyosema sheria.
vii.
Uwepo wa mpangilio usio sawa wa ujira/mishahara.
viii.
Kutopewa posho au kupewa kidogo au kutopewa kwa wakati.
ix.
Fedha za uhamisho na likizo; kwa mfano kuna walimu ambao wameanza kazi 2004
NIT Shule ya msingi Dar es Salaam wamelipwa fedha za likizo mara moja mwaka
2012, mfano halisi ni mwalimu Ruth Natumwa, huyo ni kati ya walimu hao.
Matatizo ya walimu kimsingi ni janga la taifa, yapo Taifa zima, kwa mfano
katika shule ya Sekondari Kizota, Dodoma kuna walimu wengi wana madai yao
dhidi ya Serikali, waliajiriwa mwaka jana Machi, wakaanza kupata mshahara
mwenzi wa tisa…walilipwa mshahara wa mwezi wa tisa tu na kuendelea, ile
mingine wanaendelea kudai.
x.
Mazingira magumu ya kazi mijini na vijijini (tunapozungumzia mazingira
magumu inahusisha kutokuwepo vitendea kazi au kuwa vichache, miundo mbinu duni
nk).
xi.
Waajiri kutochangia mifuko ya jamii
xii.
Fedha za makato ya wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii zimekuwa zikikopeshwa
watu wengine wasio wanachama wakiwamo wanasiasa huku wafanyakazi wenyewe
wakiendelea kuwa na maisha duni.
xiii.
Kufanya kazi kama kibarua kwa miaka mingi jambo ambalo ni tofauti za sheria
za kazi.
xiv.
Huduma za kifedha kuwa mbali na maeneo ya kazi, hali inayosababisha
wafanyakazi kutumia fedha nyingi kufuatilia mishahara kwa vile ni mbali na eneo
wanalofanyia kazi.
xv.
Kutokuwa na mfumo unaoeleweka wa upandishaji vyeo na ujira/malipo kwa
wafanyakazi/vibarua.
xvi.
Waajiri hasa binafsi kufukuza wafanyakazi hovyo/no job security…kufanya kazi
bila mikataba
xvii.
Kupambana na tatizo la kodi kubwa kwa mishahara (PAYE).
xviii.
Tatizo la mabosi kutoa upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wafanyazi kwa sababu
zisizo za kitaalamu; wakati mwingine ni kwa sababu ya ngono; kuwataka kimapenzi
wafanyakazi ili waendelee kuwepo kazini au kupandishwa vyeo, tatizo hili
linaonekana kuwa sugu, wanawake wengi maofisini hawako huru sana, wamekuwa
wakitakwa kimapenzi mno na mabosi wao, wengi wanashindwa kujizuia, tunataka
kuona kunakuwa na sheria kali dhidi ya mabosi wa aina hii kama ilivyo katika
nchi nyingine.
Tatizo la ajira
kuporwa na wageni
Ingawa sheria/sera
za ajira zinaeleza wazi kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini zaidi ya
watano kwa kazi ziziso na ujuzi, baadhi ya makampuni yamekuwa yakiingiza wageni
kwa kazi ambazo Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.
Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na
kuomba CV za wageni.
Ili tuone kama ni
kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora nafasi za Watanzania.
Nitapigania
kuhakikisha tabia ya waajiri kulazimisha waajiriwa lazima wawe na uzoefu mkubwa
inapungua au kukoma kabisa
Kigezo cha kupata
ajira kiwe ni uwezo wa mtu wakati huo baada ya kufanyiwa usaili, siyo lazima
awe na uzoefu wa miaka mitatu au mitano kama ambavyo waajiri wengi
wanalazimisha; tunahitaji kuona Serikali inasimamia hili. Kama hali ni hii,
wahitimu wanawezaje kupata ajira? Ni suala ambalo nitakuwa mkali nalo mno kwa
sababu lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania, limekuwa ni sababu ya rushwa
ikiwamo ya ngono…walioko vyuoni wengi hawana uhakika wa ajira, kwa sababu ya
tabia hii. Ni lazima tubadilike, watu waajiriwe kulingana na uwezo wao wa kazi,
siyo uzoefu.
Wanafunzi shule
ya Msingi/Sekondari nk wapatiwe elimu ya kujiajiri.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa nk.
Nitaanzisha
idara mbili mpya na kuboresha zilizoko;
i. Idara ya
walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa.
Tutaangalia
namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair
Foundation www.wheelchairfoundation.org.
Idara ya pili ni
Idara ya fursa/Career Development
Department na Mafunzo
Nimetembea katika nchi tofauti
Duniani ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius, India, Thailand,
Sweden na Marekani.
Nimeona fursa kadhaa ambazo
zimenishawishi kuanzisha idara maalum ya kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa
zinazoendelea Duniani na hapa nchini.
Fursa hizo zitakuwa zinapatikana
katika tovuti za TUCTA na ofisi za vyama vya wafanyakazi mikoani.
Baadhi ya fursa ni namna gani mtu
anaweza kusoma nje ya nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi,
fursa ya mashirika ambayo yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali.
-Kwa mfano kuna mashirika kama www.nuffic.nl
au vyuo ambavyo mtu anaweza kusoma bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu
ya Marekani na fursa nyingine nyingi.
Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki
sana na fursa hizi. Ziko pia taasisi nyingine zinatoa.
Napenda kuchukua
fursa hii kutoa onyo kwa wanaopanga kutoa rushwa kwenye huu uchaguzi wa TUCTA
kuwa tuko makini na hili tumejipanga, tutachukua hatua za haraka za kisheria
dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwaripoti kwenye vyombo husika, Rushwa si
kipaumbele utapinga kwa nguvu zetu zote.
Ndugu Dismas Lyasa
pia atasaidia kuanzisha kituo au kushirikiana na mashirika mengine kutoa
masaada wa kisheria kwa wafanyakazi wanaofukuzwa makazini kinyume cha sheria.
Wafanyakazi wengi wakikumbwa na matatizo wafanyakazi wenzao wanawatenga, vyama
vyao vinawatenga, Dismas atahakikisha kuwa TUCTA ni kimbilio lao.
Ndugu Dismas Lyasa
atasaidia kutoa mafunzo ya kisheria kwa wafanyakazi ili waweze kutambua haki
zao za msingi, kwa kuendesha semina, makongamano na mijadara itakayotoa elimu
na kuibua mijadara kwa wafanyakazi.
CHAGUA DISMAS
LYASA KWA TUCTA MPYA, Mabadiliko ni sasa, Asanteni.
No comments:
Post a Comment