Watuhumiwa wa mlipuko katika mgahawa wa kihindi wa Verma Traditional Indian Cuisene jijini Arusha wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha. (Picha na Mahmoud Ahmad)
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
WATU sita wanaotuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu kwenye mgahawa wa kihindi wa Verma Traditional Indian Cuisene jijini Arusha uliojeruhi watu nane leo wamefikishwa mahakamani.
Watuhumiwa hao ambao walifikishwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Arusha mbele ya Hakimu Anna Ngoka walisomewa mashtaka manne tofauti na mwendesha mashtaka wa serikali Augustino Kombe.
Akisoma mshtaka hayo mwendesha mashtaka wa serikali Kombe aliwasomea washtakiwa wanne ambao ni Athuman Hussen Mmasa, Jaffari Hashimu Lema, Said Michael Temba na Shaban Mmasa wanahusika na kosa la kwanza la kula njama za kutenda kosa la kigaidi kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi.
Mwanasheria wa serikali Kombe aliambia mahkama kuwa watuhumiwa hao tena wanahusika na kosa la pili ambalo kinyume na sheria za ugaidi walilipua bomu kwenye mgahawa ujulikanao Verma kati ya July 7 na 8 mwaka huu na kujeruhi watu nane.
Watuhumiwa namba 2 Athuman Mmasa na na namba 4 Jaffari Lema mwansheria Kombe alisema uwa wahusishwa na kosa la tatu ambalo ni kugawa silaha aina ya bomu na kufadhili kwa fedha kutendeka kwa tukio la kigaidi katika mgahawa Verma.
Ambapo mwanasheria huyo aliwataja watuhumiwa wote sita ambao ni Jaffari Lema, Shabana Mmsa, Athuman Mmasa, Mohamed Nuru, Said Temba na Abdul Humud ‘wagoba’ wanahusishwa na kosa la sita kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi.
Baada ya mashtaka hayo mwanasheria aliomba mahakama ipange siku ya kutajwa tena kwa shauri hilo kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka.
Hakimu Ngoka aliahirisha kesi hiyo hadi august 6, mwaka huu na kwamba washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za namna hiyo.
Awali bomu lilidaiwa kulipuka kwenye mgahawa wa chakula cha asili ya kihindi wa Verma Indian Traditional Cuisene july 7 mwaka huu saa 5 usiku na kujeruhi watu nane wote wakiwa na asili na kiasia.
Majeruhi hao walitajwa kuwa ni Deepak Gupta ambaye alikatwa mguu baada ya kujeruhiwa vibaya na mlipuko huo, Ruitik Khanehvial, Manci Gupta, Mahush Gupta, Marisa Gupta, Vinod Suresh na Prateek Javey na Raj Rajin.
Jeshi la polisi liliahidi kuwasaka kwa udi na uvumba watu waliohusika na bomu hilo na kuweza kuwafikisha kwenye mkono wa sheria na kazi imeanza kuonekana baada ya leo kuwafikisha watu sita kuhusiana na tukio hilo.

No comments:
Post a Comment