HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2014

'USIKU WA NANI KAMA MAMA' WAMPA UCHUNGU DIMPOZ



NA ELIZABETH JOHN
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema mashairi aliyoimba katika wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ alioshirikishwa na Christian Bella aliandika akiwa anamaanisha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa shoo hiyo ambayo iliandaliwa maalum kwaajili ya wimbo huo ikijulikana kama ‘Usiku wa Nani Kama Mama’, alisema anatamani mama yake angekuwepo angeona mafanikio aliyoyapata kupitia muziki.

“Mama yangu alitangulia mbele za haki, huwa natamani sana angekuwepo ili aone mafanikio niliyoyapata kupitia muziki kama wengine wanavyoona mafanikio ya watoto wao, mashairi ya wimbo huu nilikuwa namanisha sio wimbo ni maneno ambayo yapo na kila siku huwa namuombea apumzike salama,” alisema nyota huyo kwa uchungu.

Dimpoz aliwataka wasanii ambao wamekuwa wakipata mafanikio na wazazi wao wakishuhudia, kuwajali na kuwatunza kwa moyo wote kwasababu ndio chanzo cha mafanikio yao.

Dimpoz kwasasa anatamba na ngoma yake ya ‘Ndagushima’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio licha ya kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Pages