HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2014

DIAMOND AOMBA SAPOTI TUZO ZA IRAMWA

NA ELIZABETH JOHN

BAADA ya kutajwa kuwania tuzo za IRAMWA (International Reggae and World Music Awards), za nchini Marekani, nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasseb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameomba wadau wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti.

Mtanzania mwingine aliyetajwa katika tuzo hizo ni msanii wa dancehall, Dabo ambaye ametajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha 'Best New Entertainer'.

Diamond alitajwa kuwania tuzo hizo kupitia ngoma yake ya ‘Mdogo Mdogo’ katika  kipengele cha 'The Best African Song/Entertainer' akichuana na mkali kutoka Nigeria, Davido kupitia ngima yake ya ‘Aye’, Awilo Longomba (Bendeke), Willy Paul Msafi (Tam Tam), Eddy Kenzo (Sittya Loss), na Bracket (Mama Afrika).

Diamond ambaye sasa yupo nchini Marekani alipoalikwa kutumbuiza, kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika kuwa sapoti ya Watanzania ni muhimu kumuwezesha yeye kuchua tuzo hiyo. Upigaji kura tayari umeshafunguliwa na tuzo hizo zitatolewa Oktoba 4, mwaka huu nchini Marekani.

Hivi karibuni Diamond alipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kwa kunyakua tuzo ya AFRIMMA mwaka huu zilizofanyika Julai 26, Eisemann Center Richardson, Texas nchini Marekani akichaguliwa Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Pages