HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 18, 2014

FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa ofisi.

Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidikushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Mwanzoni mwa mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya jiji ili kupisha maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwamichezo na vitega uchumi.

Akiongea mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa FIFAanayeshughulikia Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema FIFA inaunga mkono wazo la kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidiakwa awamu uboreshaji huo.

Katika kuhakikisha usimamizi na utekelezajibarabara wa mradi huo, ujumbe huo wa FIFA ulikubaliana na Kamati yaUtendaji ya TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo la utawala lianzekutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.

Pamoja na kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huouliokuwa nchini kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi yakujadiliana na TFF kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali yakiwemo yaUtawala, Fedha, Masoko, Ufundi, Mashindano na timu za taifa.

Akiongea kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliushukuru ujumbe huo wa FIFA kwa msaada mkubwa katika historia ya mahusiano kati ya FIFA na TFF.
Ujio huo unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa FIFA. Mradi wa Performance unaoshirikisha nchi mashirikisho 163 kati ya wanachama 209 wa FIFA, unalenga kuongeza ufanisi
katika uendeshaji na uongozi wa nchi wanachama wa FIFA.

No comments:

Post a Comment

Pages