Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya
Maafa (TANDREC), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akiongoza
Kikao Maalum cha Kamati ya Taifa ya Maafa(TANDREC) ambayo, inaundwa na
Washiriki wakuu katika kukabili Maafa, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa
mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar
es Salaam .
Mkurugenzi Msaidizi Dharura na
Maafa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Elias Kwesi, akiwaeleza wajumbe wa
Kamati ya Taifa ya Maafa (TANDREC) jinsi walivyojidhatiti kuzuia na kukabili ugonjwa wa Ebola hapa nchini ambapo alibainisha
kuwa hakuna maabukizi ya ugonjwa huo
hapa nchini hadi sasa, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka, Kikao kimefanyika leo katika ukumbi wa
mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya
Maafa (TANDREC) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (watatu
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara
baada ya kumaliza kikao hicho leo katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri
Mkuu, Jijini Dar es Salaam .
No comments:
Post a Comment