HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 14, 2014

COASTAL UNION KUKIPIGA NA HANDENI CITY KESHO



TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga kesho  inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Handeni City mchezo unaotazamiwa kuchezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani hapa,Ofisa habari wa Coastal Union Oscar Assenga amesema mchezo huo utaanza kesho saa kumi jioni lengo likiwa ni kujenga undugu baiina ya timu zote mbili.
Assenga amesema katika mchezo huo kikosi kinachotazamiwa kushiriki ligi kuu msimu ujao kinaonyesha makali yake kwenye mchezo huo.
Aidha mashabikki wa soka mkoani hapa wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa mkali na wa kusisimua.


No comments:

Post a Comment

Pages