HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 29, 2014

Tanzania Prisons kusaka makali ya ligi kuu Sumbawanga

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

SIKU chache baada ya Mbeya City kurejea kutoka Mikoa ya Rukwa na Katavi iliko kuwa kusaka vipaji na  makali ya kujiwinda na Ligi kuu Tanzania Bara, kakazao na wapinzani wao wakuu Tanzania Prisons nao wanondoka leo kuelekea Mjini Sumbwanga kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki.

Taarifa ya iliyotolewa na Meneja wa timu hiyo Enock Lupwuto na kwamba wanaenda mjini  Sumbawana Mkoani Rukwa baada ya kupata Mwaliko na chama cha Soka Mkoa huo (RUREFA).

Akizungumza na Tanzania daima jana Meneja huyo alisema kuwa safari  itaanza leo majira ya sabui kwa basi la timu hiyo na kwamba wakiwa mjini Sumbawanga wanacheza mechi mbili ya kwanza itakuwa dhidi ya Kombain FC mchezo ambao utapigwa leo katika dimba la Nelsoni Mandela. 

Lupwuto alisema kuwa mbali na mchezo huo wa leo timu hiyo itashuka dimbani jumapili,kwa kucheza na timu ambayo watapangiwa na wenyeji wao, chama cha soka Mkoa wa Rukwa.

Meneja huo aliongeza kuwa baada ya timu yao kufanya vibaya katika msimu uliopita ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya kumi na moja,safari hiii wamedhamiria kufanya vizuri zaidi ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa msimu.

Tanzania Prisons iliyo panda daraja mwaka 1995 na mwaka 1999 ilichukua ubingwa wa ligii kuu,itaondoka leo  msafara huo utakuwa na wachezaji 27 na viongozi  5 kitajereaji jiji Mbeya Semtemba mosi
Alisema kuwa mara baada ya kurejea jiji Mbeya, msafara huo  juma tano Semptemba 3 itaondoka kuelekea jiji Dar es Salaamu ambapo itacheza michezo kadhaa ya kirafiki kabla ya ligi kuu kuanza kutimua vumbi Semptemba 20 mwaka huu.

Tanzania Prisons inayo nolewa na Devid Mwamwaja inafanya ziara hiyo ikiwa ni siku kadhaa tangu wawakilishi wengine kutoka Mbeya,Mbeya Cit FC kurejea kutoak Mikoa ya Rukwa na Katavi ilicheza michezo mitatu ikitoka sare 1 na miwili kushinda.

No comments:

Post a Comment

Pages