Mwakilishi wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas
Mwansoko (kushoto) akisalimiana na baadhi ya Wanamichezo waliokuwa kwenye
Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda
akiwaelekeza jambo baadhi ya Wanamichezo waliwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini
Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia jambo na baadhi
ya wanamichezo walikuwa wamewakilisha nchini katika mashindano ya Jumuiya ya
Madola mjini Glasgow Scotland mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko Akizungumza kwa
niaba ya Serikali na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya
Madola mjini Glasgow Scotland mara wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam jan.Kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert
Bayi.
Katibu wa Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akizungumza na wanamichezo waliokuwa
kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland wakati wa hafla
fupi ya mapokezi iliyofanyika jana
katika Ukumbi uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.wa tatu kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda na Meneja wa Uwanja wa
Taifa Bw. Rish Urio.
Mwakilishi wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akikabidhiwa Bendera ya Taifa na
Kapteni wa Timu ya Taifa iliyoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw.
Seleman Kidunda, mara baada ya kurejea nchini jana jijini Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana
Yassoda, Meneja wa Timu hiyo Muharami Mchume na Katibu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi
Baadhi ya
wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow
Scotland, wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere mara baada
ya kuwasili nchini jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow
Scotland, wakifuatilia hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali (hawapo
pichani)wakati wa hafla fupi ya mapokezi na kuwakaribisha iliyofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA
Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniI
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
No comments:
Post a Comment