Kaimu Makamu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo anayeshughulikia masuala ya Fedha Utawala, Dk. Elifuraha Mtaro (kulia) akimkabidhi barua ya udhamini wa mafunzo ya masomo ya haki za binadamu, mwanafunzi wa chuo hicho, Wilfred Madigo. Hafla hiyo ilifanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa masomo hayo kutoka Akiba Uhaki Foundation ya Nairobi Kenya, Kepta Ombati. (Picha na Francis Dande)
Na Happiness Katabazi, UB
CHUO Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Dar Es Salaam, kimendaa Mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo mpana watetezi wa Haki za Binadamu toka nchi tano za Afrika Mashariki.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Mradi Kitivo Cha Sheria Cha Chuo hicho, Teddy Sawaya alisema kuwa mafunzo hayo yamefadhiliwa na Akiba Uhaki Foundation ya Nairobi Kenya, na jumla ya wanafunzi 10 watashiriki mafuno hayo.
Sawaya ambaye ni Mhadhiri wa Sheria wa UB, amesema washiriki wa kozi hiyo ni watu wanaotokea Katika Taasisi zinazojihusisha na Kazi ya utetezi wa Haki za binadamu na kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wigi mpana zaidi Katika eneo Hilo la utetezi wa Haki za binadamu, watetezi Hao wa Haki za binadamu na Jamii kwa ujumla.
Alisema Tayari washiriki wameishathibitisha kushiriki Mafunzo hayo na kwamba Mafunzo hayo hatakuwa yakiendeshwa ndani ya madarasa la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo yaliyopo Kawe Beach Dar Es Salaam na Mafunzo yataanza rasmi Septemba 8 mwaka huu ambapo yatafunguliwa ramsi na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtaro mafunzo hayo yatamalizika Februali 22 Mwaka 2015.
Hii ni Mara ya pili kwa Chuo Kikuu cha Bagamoyo , kuendesha Mafunzo hayo ya utetezi wa Haki za binadamu kwa kuudhuliwa na washiriki toka nchi tano za Afrika Mashariki. Mara ya kwanza UB iliendesha kozi hiyo Septemba 8- Oktoba 20 Mwaka Jana.
No comments:
Post a Comment