Wanamuziki Vanessa Mdee, Jo Makini na Shaa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye 'red Carpet wakati wa uzinduzi huo.
Mwanamitindo
Rio Paul (kushoto) akiwa na rafiki zake muda mfupi baada ya uzinduzi wa
msimu wa pili wa Coke studio Africa, Hyatt Hotel, jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola,
jana usiku ilizindua msimu wa pili wa onyesho la runinga
lijulikanalo kama ‘Coke Studio Africa’ ambalo
linatarajiwa konyeshwa kila Jumatatu na kituo cha Shirika la Utangazaji cha TBC.
Akizungumza na wandishi wa habari
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijijini
Dar es Salaam, Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema, ni
furaha na fahari kwa watanzania na waafrika kwa ujumla kwa kukutana pamoja na
kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo, ambapo watu watapata kuona na kujifunza
vipaji na radha nzuri kutoka kwa wasanii 24 wa bara la Afrika.
“Muziki ni lugha isiyo na mipaka
na njia muhimu ya kuonyesha hisia na furaha, tungependa kusambaza furaha Barani
Afrika kupitia muziki kwa kushirikiana na wasanii,” alisema Njowoka.
Alisema, ujumbe wa msimu wa mwaka
huu ni ‘Ushirikiano wa Afrika, muziki wa
afrika’, ambapo pia mbali na wasanii nyota pia wameweza kushirikisha bendi,
watayarishaji muziki na madj bora wa bara la Afrika.
Njowoka aliwataja wasanii hao kwa
mwaka huu na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na Flavor Nabania, Omawumi, Waje, Burna Boy, Chidima,
Olamide, Iyanya, Seyi Shay,Yemi Alade na Phyno (wote kutoka Nigeria), wengine ni Fena Gitu, Rabbit, Victoria Kimani
na Jay A (Wote kutoka Kenya), Navio,
Jacie Chandiru na Lilian Mbabazi (Kutoka Uganda), John Makini, Shaa, Diamond na Vanessa Mdee (Kutoka
Tanzania).
Wengine ni Neyma, Jose Valdemiro na
Marllen (Msumbiji) huku watayarishaji wa muziki ni Silvastone (Ghana),
Chopstix na Afrologic (Nigeria), Kevin Provoke, Kagwe Mugai na Owuor Arunga
(Kenya) na wengieo.
Hata hivyo, mbali na kuonyeshwa
kila Jumatatu kupitia runinga ya TBC,
mashabiki wanaweza kufuatilia pia kupitia tovuti ya Coke studio ambayo
ni www.cokestudioafrica.com.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na
mastaa mbalimbali wakiwemo wanamitindo, wabunifu, mamiss, wasanii wa filamu,
muziki, vichekesho.
No comments:
Post a Comment