HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 27, 2014

COASTAL UNION YAIPA USHAURI TFF KUHUSU VITENDO VYA KISHIRIKINA VIWANJANI

Na Mwandishi Wetu,Tanga

KLABU ya Coastal Union imelishauri shirikisho la soka nchini(TFF) kuhakikisha wanakuwa wakali kwenye kidhitibi vitendo vya kishirikina ambavyo vinajitokeza kabla ya kuanza michezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara kwani hali hiyo inadumaza maendeleo soka hapa nchini

Kwa sababu hali hiyo isipodhibitiwa upo uwezekano mkubwa wa timu za Tanzania kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa wanayocheza nje za nchini

Kauli hiyo imetolewa leo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Albert Peter mara baada ya usiku wa jana saa saba usiku mashabiki ambao inasadikika ni wa timu ya Mbeya City kumwaga madawa kwenye kambi ya Coastal Union jambo ambalo sio zuri.

Mjumbe huyo ambaye pia  ni Mkuu wa Msafara wa Coastal Union amesema jambo hilo linapaswa kukemewa ikiwemo kuchukua hatua kali timu ambazo zitabainika zimefanya mambo ya kishirikina ili kuweza kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao.

 Amesema kuwa jambo hilo la mashabiki kufanya vitendo vya kishirikina kabla ya mechi hi suala ambalo sio zuri kwa sababu linapelekea kushusha kiwango cha soka hapa nchini hivyo iwekwe sheria kali kwa timu itakaobaini imefanya hivyo kuchukulia hatua ili kukomeza vitendo hivyo.

Licha ya hayo amesema kikosi cha timu hiyo kimejipanga vizuri ili kuweza kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages