HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 08, 2014

LAPF YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA WANACHAMA WAKE

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
 Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Vijana kutoka Kigamboni Community Centre wakitoa burudani ya ngoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ huduma mpya ya mikopo ya eilimu ya juu kwa wanachama wa LAPF, iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu ‘Piga Kitabu na LAPF’
 Uzinduzi rasmi wa Piga Kitabu na LAPF ulipambwa na shamrashamra za aina yake.
 Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akimkabidhi mfano wa hundi Bwana Rolland Lyamuya mmoja wa wanachama wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambaye amenufaika na huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu ‘Piga Kitabu na LAPF’  iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Piga Kitabu na LAPF Mh. Hawa A. Ghasia akipokea zawadi ya kitabu cha Nelson Mandela kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Kalunde Band wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Pages