Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati
ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji
kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi
kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi
hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi
kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda
kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua
kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao
wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia
tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo
na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili
limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba
na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu
yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha
za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi
kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa
kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya
Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba
19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.
No comments:
Post a Comment