Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Coastal Union ya Tanga “Wagosi wa Kaya” ambayo ilikuwa icheze mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar
Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mchezo huo umesogozwa mbele sasa kucheza Jumapili katika Uwanja wa
Mkwakwani ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara ambao unatarajiwa kuanza Septemba 20 hapa nchini.
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa sababu ya kuwepo kwa
mechi za uingereza Jumamosi
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar
Assenga amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na tayari
walishafanya mazungumzo na uongozi wa wakata miwa hao hivyo watawasili mkoani
hapa siku moja kabla ya mchezo huo.
Assenga amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni wa pili
kwa timu ya Coastal Union kucheza ikiwa mkoani hapa baada ya kurejea kutoka
Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matayarisho
ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema baada ya mchezo wa kwanza timu hiyo kuibuka
na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro hivyo waliona umuhimu wa mechi
hiyo lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho kabla ya kuwavaa wekundu wa
msimbazi Simba siku ya ufunguzi wa Ligi kuu.
Ameongeza kuwa wanategemea mechi hiyo itakuwa na upinzani
mkubwa sana hivyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake watumia fursa hii kuja
kuiona timu yao ya Coastal Union ikipambana kwenye mchezo huo kabla haijaanza
msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Hata hivyo amesema kuwa msimu huu timu hiyo imepania
kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi zake za nyumbani na ugenini ili kuweza
kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara .
No comments:
Post a Comment