Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA) yafanyika Wilayani Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw.
Wilman Ndile afungua Warsha ya Siku Mbili Wilayani Mtwara kuhusu “Mpango wa Kujikinga, Kukabiliana na
Kuzuia athari za Maafa kwa Wilaya ya Mtwara leo tarehe 26 na 27 Septemba, 2014.
Wakati wa ufunguzi huo Bw. Ndile alisema Mpango huu utasaidia sana pindi maafa
yatakapotokea na kuwaomba washiriki wa warsha hiyo kutoka Manispaa na
Halmashauri ya Wilaya hiyo kushiriki vema katika mafunzo na kuchangia masuala
hayo ili kuweza kukamilisha mpango huo unaoratibiwa na Idara ya Uratibu wa
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema “hatua hizi
zimekuwa madhubutu na zitatusaidia sana sisi kama wadau wakubwa wa Maafa katika
Halamshauri zetu na Manispaa kwa kuona uzito wa
suala la Maafa ni la kila mmoja na sio Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye ni
mratibu tu wa Maafa” alisisitiza Bw. Ndile.
Washiri wa warsha kuhusu maafa kutoka Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman M. Ndile (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya Siku mbili inayoratibiwa na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa yaani (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA)
Imetolewa na Afisa Habari
Ofisi ya Waziri Mkuu
26 Septemba, 2014, Mtwara
No comments:
Post a Comment