Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akifafanua jambo kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba lilivyochakachua maoni ya wananchi wakati wa hafla ya kutimiza 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wakiwa katika mkutano huo.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia (kulia).
Warioba akifafanua jambo kuhusu Bunge Maalum la Katiba.
Wageni waalikwa.
Warioba akifafanua jambo kuhusu Bunge Maalum la Katiba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk. Helen Kijo Bisimba (kushoto), Askofu Elinaza Sendoro na Prof. Chris Maina (kulia).
Washiriki.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizindua kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na Dk. Sengondo Mvungi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba, Askofu Elinaza Sendoro, na Prof. Chris Maina wakionyesha kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na marehemu Dk. Sengondo Mvungi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo Bisimba akionyesha kitabu cha Breathing the Constitution kilichoandikwa na marehemu Dk. Sengondo Mvungi. Kulia ni Askofu Elinaza Sendoro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MWENYEKITI wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema kwa hali ya mambo yanayoendelea bungeni haoni
matumaini ya kupatikana kwa katiba mpya na kwamba hali hiyo imemkatisha tamaa.
Wakati jaji Warioba akikatishwa tamaa na uwezekano
wa kupatikana katiba mpya, Muhadhiri wa vyuo mbali mbali nchini Profesa Chris Peter
Maina, ameeleza kuwa watu wanaotaka kuzuia historia kuandikwa kwa kutumia
askari wa Kutuliza ghasia hawatafanikiwa kwa kile alichoeleza kuwa historia
itawaumbua watu wa aina hiyo.
Jaji warioba na Profesa Maina walitoa kauli hiyo
jana jijini Dar e sSalaam wakati wa kumbu kumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki
kwa Dk. Sengondo Mvungi, pamoja na hafla ya
kutimiza miaka 19 ya kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu(LHRC).
Katika matukio hayo mawili yaliyoendana na uzinduzi
wa kitabu cha historia ya maisha ya Dk
Mvungi Jaji Warioba alisema, tangu mwanzo matumaini yalikuwa ni nchi kupata
katiba mpya kwa maridhiano na kwamba
baada ya mchakato huo wa katiba kutekwa na wanasiasa matumaini hayo yametoweka
Alisema badala yake wanasiasa hao wameacha kuangalia
maslahi ya taifa na kutegemea uamuzi wa kura badala ya nafasi ya maridhiano
kupewa kipaumbele.
“Sina
hakika kama tutapata katiba mpya kwani
rasimu itakayopendekezwa na bunge maalum haitapigiwa kura hadi mwaka 2016 kwa
kuwa hakuna maridhiano hasa kuhusu muungano rasimu hiyo itaanza kupigwa tangu
siku ya kutolewa kwake.”alisema na kuongeza
Kampeni ya uchaguzi ya mwaka kesho katiba mpya
itakuwa agenda inayoweza kuigawa nchi.
Akiongelea rasimu iliyopitishwa n a bunge maalum la
katiba jaji Warioba alisema limepitisha rasimu yake na kuacha maoni
yaliyotolewa na wananchi na kwamba jambo hilo ni hatari
Jaji Warioba alisema licha ya baadhi ya mambo
kuonekana kukubaliwa katika rasimu hiyo ya bunge bado kuna mambo mengi ya
msingi yamewekwa pembeni na kwamba wabunge waliopitisha uamuzi huo wanapaswa
kutoa maelezo ya kutosha kwa wananchi
Aliyataja baadhi ya mambo ambayo mwelekeo wake ni
kukataliwa na wananchi kuwa ni pamoj.
Maadili
ya viongozi
Katika maadili
ya viongozi alidai kuwa wananchi walitoa
maoni mazito kuhusu maadili ndani ya
jamii na maadili ya viongozi kwa kuwa wanachukizwa na kuporomoka kwa maadili.
Kutokana na maoni ya wananchi, alisema Tume
iliimarisha misingi mikuu ya taifa iliyo
katika utangulizi wa rasimu ambako misingi katika katiba ya sasa ni uhuru, haki
udugu na amani lakini kutokana na maoni ya wananchi misingi mipya iliongozwa
nayo ni pamoja na utu,usawa, umoja na mshikanamo.
Wananchi pia walipendekeza tunu za taifa ziwekwe
kwenye katiba, tunzu hizo ni pamoja na utu, uzalendo, uadilifu,umoja, uwazi, uwajibikaji
na lugha ya taifa ya Kiswahili.
Hata hivyo Warioba alisema ni jambo la kusikitisha
kwa kuwa Bunge maalum limeondoa
uadilifu, uzalendo, umoja, uwazi na
uwajibikaji kutoka kwenye orodha ya tunu za taifa na kuziweka kwenye misingi ya
utawala bora na kuongeza kuwa kila mtanzania anapaswa awe na tunu hizo.
Madaraka
ya wananchi
Kuhusu madaraka ya wananchi alisema kuwa katiba
inatungwa na wananchi na kwa maoni yao wanataka wawe na madaraka ya kumwondoa mbunge wao kama hawaridhiki na
uwakilishi wake.
Akilifafanua hili alisema ni kweli siyo jambo la
kawaida kumwondoa mbunge katikati ya kipindi
au kumwekea ukomo, lakini kwa sababu ya rushwa katika uchaguzi wananchi
wanaona ni vema watumie madaraka yao kuwajibisha wabunge wao.
Katika hili alisema hii inawekana kwa kuwa tayari
bunge lina kanuni za kuwaajibisha wabunge, vyama vya siasa vina madaraka ya
kuwaondoa vivyo hivyo wanannchi nao wanapenda kuwa na madaraka hayo.
Mgawanyo
wa Madaraka kati ya mihimili
Warioba alisema pendekezo la kumwondoa Rais na
Mawaziri kutoka kwenye Bunge linakataliwa kwa sababau kumezoeleka mfumo wa
kibunge kama ilivyo kwa nchi za jumuiya ya madola.
“Siyo kweli kwamba mfumo wetu ni wa kibunge kwani
kwenye mfumo wa kibunge mkuu wa nchi hana madaraka ya utendaji bali madaraka
hayo yako mikononi mwa Waziri Mkuu ambaye ni mbunge na hivyo ndivyo ilivyo kwa Uingereza,
India, Canada, Australia na New Zealand.
“Ikumbukwe kwamba
Tanzania ina mfumo wa Urais ambapo rais ni mkuu wa nchi, Mtendaji Mkuu,
Amir Jeshi Mkuu hivyo Rais na Mawaziri wake kuwa sehemu ya Bunge ni kuchanganya
mamlaka ambako hali hii ndio inafanya Serikali kuingilia mamlaka ya bunge na pia bunge kuingilia mamlaka ya
serikali.
“Tumeona wakati mchakato huu wa katiba jinsi
madaraka yanavyoingiliana ambako wakati wa kutunga sheria ya mabadiliko ya
katiba tuliona jinsi bunge lilivyokuwa linafanya maamuzi ikiwa ni pamoja na
kutunga sheria.
“Lakini baadaye Rais anafanya mazungumzo na watu nje
ya bunge na baadaye bunge linalazimika kubadili maamuzi ambako hata bunge
maalum la katiba limetendewa hivyo kwa maana hiyo bunge halina madaraka kamili
na Rais anaweza kuingilia wakati wowote,”alisema Warioba.
Wakati katika Bunge la kawaida alisema mawaziri
wanawabana wabunge kupitisha mambo ya Serikali na wabunge mara nyingine
wanaingilia kazi za Serikali kwa mfano kamati za bunge kwenda moja kwa moja
kwenye taasisi za Serikali kutoa maagizo au kutoa maazimio kwa hatua
kuchukuliwa kwenye maeneo ya utendaji.
Hivyo anachoona yeye dhana ya kutenganisha madaraka
ya mhimili ni jambo la msingi sana katika mfumo wa demokrasia na nchi nyingi
zimebadili katiba ili kutenganisha madaraka na mihimili na zimefanya hivyo na
sababu zao zinafanana kabisa na zile ambazo wananchi wa Tanzania walitoa.
Muundo
wa Muungano
Katika suala la muungano ambalo ndilo limeteka
nafasi kubwa ya majadiliano tangu mchakato huo uanze, Warioba alisema pamoja na
Tume kuorodhesha kero zaidi ya 40, baada
ya uchambuzi wa kina ilionekana kero nyingi ama zimepatiwa ufumbuzi au zinaweza
kurekebishwa na tume ilichambua tu zile kero ambazo zilionekana ni nzito.
Huku akidai kuwa lalamiko kubwa kwa upande wa
Tanzania Bara ni Zanzibar kuvunja katiba ya Muungano ambako alihoji kuwa kutokana
na yale yaliyopitishwa na Bunge la sasa ni kweli Zanzibar itakubali sheria
zanazotungwa na Bunge kutumika nchi nzima bila masharti.
Swali lingine ni kama kweli Zanzibar imekubali Mahakama
ya Rufaa na Mahakama ya Juu ziwe mamlaka nchi nzima bila masharti, itakubali
kuondoa mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2010 na suala la Bunge kupendekeza kwamba
raia awe na haki kupata ardhi, je Zanzibar wamekubali raia wote wawe na haki
hiyo kwa upande wa Zanzibar.
Awasubiri wabunge mitaani
Kuhusu Shutuma mbali mbali zilizoelekezwa na wabunge
wa bunge maalum kwa wajumbe wa Tume yake, Jaji Warioba alisema baada ya wabunge
hao kumaliza kuongea katika vipaza sauti vya bunge wanapaswa kutambua kuwa
wanawasubiri mitaani
“Wao wanasema jaji Warioba na wajumbe wenzake ni
Shiidaah tena wanasema Warioba ni shida kubwa, mimi nawaambiua wanakaribia
kuacha vipaza sauti vya bunge waje huku mitaani wawaeleze wananchi yale
waliyopitisha na sisi tutabaki katika msimamo wa kutetea maoni ya wananchi hapo
ndipo watakapojia kama walio na shida ni sisi au wao”alisema Warioba
No comments:
Post a Comment