Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto),
akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda. Msaada huo wenye thamani ya sh.
milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika tamasha la Pasaka na Krismasi. (Picha na
Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.
Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.
Watoto wa kituo cha Maunga cha Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Rashid Mpinda (mwenye kofia).
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha
Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Msama akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha Tovichodo cha Temeke.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto),
akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda. Msaada huo wenye thamani ya sh.
milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika tamasha la Pasaka na Krismasi.
Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda akimshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa misaada aliyotoa.
Msama akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga.
Watoto wakimshukuru Msama baada ya kuwapatia msaada wa vyakula mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kituo cha Tovichodo cha Temeke, Honoratha Michael akipokea sehemu ya msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.
Na Francis Dande
KAMPUNI
ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex
Msama, juzi ilitoa misaada ya kiutu kwa vituo vitatu vya kulea yatima vya
wilayani Kinondoni na Temeke.
Msaada
huo ambao ni utekelezaji wa programu ya kampuni hiyo kama
moja ya kurejesha sehemu ya faida itokanayo na uratibu wa matamasha ya muziki
wa injili kwa jamii.
Msama
Promotions Ltd ambayo pia ni waratibu wa tamasha la muziki wa injili la Pasaka
na Krismas, si mara ya kwanza kwao kutoa misaada ya aina hiyo kwa vituo vua
yatima na watu wengine wenye mahitaji kama
wajane na wazee.
Vikundi
vilivyonufaika na msaada huo Jumapili, ni kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni, nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam na Maunga pia cha Kinondoni.
Aidha,
misada hiyo imewafariji watoto yatima wa kituo cha Tovichido cha Wilayani
Temeke akisema amefanya hivyo baada ya kuguswa na hali halisi inayowakabili.
Msama
alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa watu wenye uwezo, makampuni na taasisi
mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia
maisha kama wengine.
Kwa
upande wa misaada iliyokabidhiwa kwa vituo hivyo, ni mchele, sukari, unga,
mafuta ya kula, chumvi, unga wa ngano na vingine vingi kwa ajili ya matumizi ya
kila siku nyumbani, vyote vikiwa na thamani ya shilingi mil 7.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa Kituo cha Maunga, Rashid Mpinda alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada
hiyo na kuwasihi wengine waige mfano huo wa kusaidia makundi maalum.
Akielezea
changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mpinda alisema ni kukosa uwezo wa
kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma hadi kufukuzwa kwa kukosa karo, hivyo
kushindwa kupata elimu.
Msama
kwa upande wake alisema jukumu la karo za wanafunzi hao analibeba yeye pamoja
na sare kutokana na kuguswa kwake na
kilio cha watoto hao.
No comments:
Post a Comment