HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 22, 2014

NSSF YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA KWA WANACHAMA WA HIARI KUTOKA TAASISI YA PFT

Hadi kufikia sasa PFT imefanikiwa kuunda jumla ya vikundi 150 vyenye wanachama 3,865 , wanawake wakiwa 3469 na wanaume 396, wanachama hao wamewekeza jumla ya sh. 1,443,806,510 kupitia mpango wa ununuzi wa hisa za kila wiki.


Katika risala yao wanachama hao wapya wa kutoka taasisi ya PFT walisema “Bodi ya wakurugenzi ya PFT na wanachama wote wa vicoba vinavyoratibiwa na Poverty Fighting Tanzania wameiomba NSSF kupitia Saccos Scheme iwasaidie kupunguza tatizo la mitaji midogo kwa wanachama wa vicoba kwa kuwapatia mkopo ambao kwa nidhamu waliyonayo wanachama wa vicoba wataweza kurudisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano yatakayofikiwa, ilisema sehemu ya risala hiyo.

"Imani yetu ni kwamba NSSF itaendelea kushirikiana nasi na kutusaidia kupata mafao yaliyoainishwa ambayo mwanachama anastahili". 


Poverty Fighting Tanzania imeunga mkono kwa vitendo kampeni ya kitaifa ambayo NSSF ni wadau wakubwa wa “Kamata Fursa Twende Zetu”


Nae Mkurugenzi Mkuu wa NSSF. Dk. Ramadhani Dau akijibu Risala yao alihaidi kuwakopesha wana PFT kupitia NSSF SACCOS Scheme shilingi za kitanzania bilioni 1.5.

Semina endelevu za FURSA zinaendelea nchi nzima kwa udhamini wa NSSF ili kuweza kuwafikia wanachama,wa Hiari zaidi kama hawa wa PFT.

Semina hizi zinatarajiwa kusaidia kutoa elimu kwa Umma na uandikishaji wa Wanachama kwa mpango wa NSSF Hiari Scheme kote nchini ili kujikwamua na umaskini na maradhi kwa kupitia mafao ya NSSF na Pensheni.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT), akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa PTA jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Vicoba kutoka vikundi 150 vinavyoratibiwa na taasisi ya Poverty Fighting Tanzania. 
Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa PTA jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya 211 wa taasisi ya Poverty Fighting Tanzania. 
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau akiwasili ukumbini huku akifuatana na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT).
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF mwanachama wa PFT, Chiku Seleman.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF mwanachama wa PFT, Gome Christopher.
Baadhi ya wanachama wa PFT wakiwa katika mkutano huo.
Wanachamawa PFT wakicheza muziki.
Baadhi ya waachama wa PFT wakionyesha mshikamano wao.
Mwakilishi wa PFT akisoma historia ya taasisi hiyo. 
Pili Rashid Matimbwa akisoma shairi wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT), akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau  na Naibu Meya wa Temeke, Juma Mkenga.
Baadhi ya wanachama wakionyesha kadi zao za NSSF.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Poverty Fighting Tanzania (PFT), akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau  na Naibu Meya wa Temeke, Juma Mkenga.
Baadhi ya wanachama wakionyesha kadi zao za NSSF.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhan Dau akisalimiana na Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Temeke, Nour Aziz.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laHifadhi ya Jamii (NSSF) Dk. Ramadhan Dau akisalimiana na Ofisa Matekelezo wa Shirika hilo, Issa Dihenga.
Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akitoka katika ukumbi wa mkutano. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Naibu Meya wa Temeke, Juma Mkenga.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhan Dau akiagana na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.
Baadhi ya wanachama wapya wakiwa na fomu zao baada ya kujiunga na NSSF.
Wanachama wapya waliojiunga n Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakirudisha fomu kwa Ofisa Matekelezo wa Shirika hilo, Ramadhan Jumbe katika hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanachama 211 walikabidhiwa kadi zao. 
Wanachama wapya waliojiunga n Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakirudisha fomu kwa Ofisa Matekelezo wa Shirika hilo, Ramadhan Jumbe katika hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanachama 211 wapya walijiunga na NSSF katika mkutano huo. 
Ofisa Matekelezo wa NSSF, Kuluthum Ally Yusuph (kushoto), akipokea fomu za wanachama wapya waliojiunga na NSSF. Wanachama wapya 211 walijiunga na NSSF.
Kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka kujiunga na NSSF.
Pili Rashid Matimbwa akipokea kadi yake kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhan Dau.

No comments:

Post a Comment

Pages