HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2014

NAIBU WAZIRI NKAMIA AZINDUA LOGO YA REDIO TRIPLE A FM

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Radio Triple A FM inayoongozwa na Mkurugenzi Mr & Mrs Papa King Mollel baada ya kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini hapa.
(Picha na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii Arusha)

Mahmoud Ahmad, Arusha
Serekali imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia jamii bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa amani.

Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

"Lengo hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na jamii"alisisitiza Nkamia

Kwa Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi aliwakemea mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo pia kupachika picha zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja

Matindi alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata maadili hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka taaluma na weledi wa tasnia hiyo

Naye meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza Triple A Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa sekta mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii

Mkurugenzi wa The Blue Triple A Ltd Papaa King aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha kuwa Redio hiyo itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo kuwapa maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango .

No comments:

Post a Comment

Pages