Wananchi wa Mbagala Kuu ambao waliathilika na mlipuko wa mabomu
katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Aprili 2009 wakiwa na mabango yenye ujumbe wa
kumtaka Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio chao baada ya kufanyiwa unyama na
viongozi waliosimamia zoezi la malipo yao.
Wananchi wa Mbagala Kuu Waathilika na Mabomu wanaamini wametolewa Kafara kwa viongozi waliosimamia malipo kwa kunufaika kupitia matatizo yao.
Mh. Rais wananchi wanasema toka ulipokwenda mbagala Kuu februari 2010 hakuna kilichofanyika zaidi kulipwa kiasi cha Tsh 1,400 na 1950 fidia ya nyumba je hii ndiyo HAKI? Rais.
Wanasikitika kwa kutotendewa haki ya kibinaadamu.
Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulalamikia malipo ya dhuluma.
Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulalamikia malipo ya dhuluma.
Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulalamikia malipo ya dhuluma.
Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulalamikia malipo ya dhuluma.
Hundi ambazo siyo sahihi kwa malipo ya waliopoteza nyumba wa watu na mali huu siyo Ubinadamu madaraka yana mwisho.
Hundi ambazo siyo sahihi kwa malipo ya waliopoteza nyumba, watu na mali huu siyo ubinadamu madaraka yana mwisho.
Na Asha Mwakyonde
Na Asha Mwakyonde
ZAIDI ya waathirika 1000 wa milipuko ya mabomu ya Mbagala
Kuu iliyotokea jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wanatarajia kuitisha mkutano wa
hadhara wa kuwaondoa madarakani viongozi wao wa serikali ya mtaa kwa madai ya
kushindwa kusimamia madai ya kupunjwa fidia ya majengo.
Wamesema licha ya miongoni mwao kulipwa fidia ya shilingi 1,400
kwa nyumba bado viongozi wao wa mtaa
wameendelea kuwa kimya katika kufuatilia fidia halisi tangu janga hilo la
mabomu liwakute miaka minne iliyopita.
Wakazi hao wa Mbagala Kuu, walitoa kauli hiyo jana walipokuwa
wakizungumza na waandishi wa habari na kusema wamefikia uamuzi huo baada ya
kukosa imani na viongozi wao.
Akizungumza kwa niaba ya waathirika wa mabomu hayo katibu
wa Kamati ya Waathirika, Thomas Mbasha, alisema madai yao ni pamoja na kulipwa
fidia ndogo na kwamba hata baada ya kuandika barua ya malalamiko kwa serikali wakitaka kuongezwa fidia lakini
hawajapata majibu yenje tija.
“Tumeandika barua kadhaa kwa serikali ikiwa ni pamoja na
Rais tukiomba fidia zetu lakini hakuna kilichofanyika,tunahitaji Rais aingilie
kati suala hili na kutusaidia ili tulipwe stahili zetu kabla hajaondoka
madarakani,” alisema Mbasha.
Alisema fidia walizolipwa awali hazilingani na thamani ya
mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo huku akiainisha fidia ya
kiwango cha juu walicholipwa ni shilingi 4900 .
Awali Mwenyekiti wa
Kamati ya waathirika wa mabomu ya Mbagala kuu, Stephen Gimonge, alisema Rais
Jakaya Kikwete, alitembelea eneo hilo na kuahidi kuwa serikali itawalipa fidia
inayostahili lakini ahadi hiyo haijazaa matunda.
Alisema wakati wa ziara yake kwa waathirika wa milipuko ya
Mbagala Rais Kiwete alimuelekeza Waziri Mkuu kuhakikisha fidia inatolewa kulingana na mali zilizopotea.
Hata hivyo
waathirika hao walimuomba Kikwete kuingilia kati ili awasaidie waweze kupata
fidia inayostahili kutokana na mali na vitu vyao vilivyoharibiwa wakati wa
tukio hilo lililotokea Aprili 2009.
No comments:
Post a Comment