MOJA ya sifa ya mwandishi ni kusoma,
na katika kusoma huko na kupekua pekua hapa na pale unaweza kujifunza na kupata
la kuandika kupitia maandiko ya watu wengine na kutoa elimu kwa umma. Leo
nimepita pita katika kurasa za marafiki zangu huko katika uso wa kitabu ‘Facebook
nikakutana na nasaha ya ndugu yangu Victory Richard, juu ya kuwasihi wanawake kwamba
sasa wavae nguo.
Ndugu
yangu yule amechoshwa na tabia
za dada zetu, wake zetu na hata mama zetu wakati mwingine wanavyotembea
uchi, ndio! utavaaje nguo fupiii au skintight halafu useme umevaa nguo?.
Binafsi naomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza mtu hasa hao mama zetu,
Ah! Lakini
potelea mbali Anko Kidevu sijali kitu si wamejitakia.
Hivi akina mama na dada zetu kweli
jamani katika yooote ambayo mnalilia usawa na sisi tunakubali kuwa sawa, hili
la kutembea uchi au kuvaa mavazi nusu uchi mbona mnapitiliza?
Ndio mmepitiliza Anko nimebaini kuwa
mmetupita maana sisi tukivaa sana ni kaptura au bichkoma na kawosh au singlendi
lakini sasa naona mmepita katika sketi na sasa mna vimini na kuacha vifua wazi.
Ni nani awezaye kuona aibu yenu
zaidi yangu mimi Anko Kidevu na kaka yenu Victor Richard, tafadhalini
tunawasihi, hebu vaeni nguo sasa na jamii itawaheshimu maana hakuna heshima kwa
mwanamke hata kidogo. Na kama mnahisi mnaheshimika kwa hilo ni bure kabisa. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG
No comments:
Post a Comment