Na
Bryceson Mathias, Morogoro
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaonya Wakulima Morogoro, wasikubali
kudanganywa na Siasa za Chama cha Mapinduzi (CCM), ili kumkopesha Mazao yao Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa ahadi ya
kulipwa fedha zao baadaye.
Akizungumza na Gazeti hili Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda
Maghorofani,
Elizeus Rwegasira, alisema, kuna na Madai ya baadhi ya Vigogo wa Serikali
wamejigeuza Wachuuzi wa Mazao hayo, hivyo NFRA inawapendelea kuwapa Magunia na
kuwatosa Wakulima Walalahoi.
“Hali
ya Wakulima walalahoi ni mbaya, hawajitambui kuwa wanaendelea kupewa Ulaghai na
CCM bila kujua cha kufanya juu ya mauzo ya mazao yao. Chadema tunawashauri,
Wanaweza kuuza kwa wanunuzi wa kawaida au kusubiri mwelekeo mzuri wa Mahitaji
na Ugaviwa Soko.
“Msirubuniwe
na wanasiasa uchwara Msisubiri Mahitaji na Ugavi wa Soko (Demand and Supply)
Mtalia kilio kibaya, maana kinachoonekana sasa, baadhi yao wanatumia fedha ya
Serikali ya NFRA kununua mazao yao, wajinufaishe wao na ndugu zao”.alionya
Rwegasira.
Meneja wa Kanda wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),
Emmanuel Msuya, alikanusha NFRA kuwapa Upendeleo Vigogo wa Serikali Magunia ya
Mahindi ili kubeba wao na ndugu zao wauze Mahindi yao, isipokuwa alidai
wanaowapa ni Mawakala wao waliosajiliwa.
Kauli hiyo ilipingwa na Wakulima wakidai, Serikali ilishatangaza
mahhindi hayawezi kuuzwa kwa Mawakala isipokuwa iyanunua moja kwa moja kwa
Wakulima, jambo ambalo Viongozi wa NFRA wanakiuka kwa kuwapendelea vigogo
kuwapa magunia
wauze mazao yao.
“Utaratibu
upo wazi, kwamba mahindi ya mkulima ndiyo yanapaswa kupewa kipaumbele, na
Serikali imeliagiza hilo, lakini cha kushngaza mahindi ya Mawakala pamoja na
wachuuzi ndiyo yanayopewa nafasi kubwa jambo ambalo hatukubaliani nalo kabisa”,
alisema Mkulima aliyeomba asitajwe.
No comments:
Post a Comment