HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 15, 2014

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ATAKA MAZAO YA WAKULIMA YANUNULIWE ILI KUWAONGOZEA KIPATO WAKULIMA


 Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagana na wanavikundi vya uchumi wa Kijiji cha Lugagala wakishangilia ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo katika kijiji pao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la uanzishwaji wa majengo ya vikundi vya uchumi katika kijiji cha Muungano Zomba Mkoani Ruvuma.
 Balozi Seif akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Lugagala kata ya ilagano Mkoani Ruvuma.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye Mkutano wa Hadhara kwa ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Makamanda wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa ndege wa Songea mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaendelea na juhudi zake katika kuona mazao ya wakulima vijijini hasa chakula cha nafaka (Mahindi) yananunuliwa ili kuwaongezea uwezo wa kimapato wakulima hao katika kukabiliana na ukali wa maisha. Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa

  Kijiji cha Lugagala kwenye mkutano wa hadhara baada ya
kushiriki kazi za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho
  pamoja na kuweka jiwe la msingi la nyumba za miradi ya
  vikundi vya uchumi katika Kijiji cha Muungano Zomba akiwa
katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za
kiuchumi, ustawi wa jamii na maendeleo.

Alisema Serikali haiwezi kuona nguvu za Wananchi zina potea
  bure bila ya kuunga mkono hasa ikizingatia kwamba asilimia
90% ya Watanzania wote wanaishi katika maeneo ya uzalishaji
vijijini.

Alifahamisha utafiti na uchunguzi wa kina utafanywa kupitia
Halmashauri za Wilaya zinazohusika na uzalishaji wa mazao
hayo ya biashara ili kuwadhibiti walanguzi wenye tabia ya
  kuwanyhonya wakulima kwa ujanja wa kununua mazao yao kwa bei ya chini.

“ Serikali haitokubali kuwaachia walanguzi kuendesha
  mpango wa kuwanyonya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ya chini na wao wakaiuzia Serikali kwa bei ya juu “.
Alisema Balozi Seif.

Balozi Seif alieleza kuwa tathmini itafanywa ili msimu ujao
wa kilimo cha nafaka wakulima watendewe na kukamilishiwa
haki zao ili kupewa nguvu na ari zaidi ya uzalishaji.

  Akizungumza na wana vikundi vya Kijiji cha Lugagala Makamu
  wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wananchi wa Kijiji
cha Muungano Zomba  kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi
  vitakav yowakomboa kiuchumi hapo baadaye.

Balozi Seif alisema uwamuzi wa wananchi hao kuanzisha
vikundi hivyo umekuwa ni jambo la busara wakielewa
  kwamba  suala la ajira ambalo huwakumba zaidi vijana
limekuwa gumu  hasa katika sekta za umma.

  Aliwataka wana vikundi hao lazima wawe makini katika
  mikutano yao ya tathmini kwa kuondoa urasimu na wawe wazi
jambao ambalo litaleta kuaminiana baina ya wana vikundi
hao.

  Kuhusu suala la Katiba Mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalum
la Katiba Balozi Seif alisema viongozi pamoja wabune wenyewe
waliousika na mchakato wa kupati,kana kwa Katiba hiyo
wataendeleza juhudi katika kuwapatia elimu wananchi kujua
faida ya kuipigia kura wakati utapowadia.

Alisisitiza umuhimu wa kudumishwa kwa amani iliyopo Nchini
  kwa vile makundi yote yaliyoshiriki mchakato huo yameonyesha
kuridhika la Katiba hiyo inayopendekezwa.

Balozi Seif aliongeza kwamba wananchi wakati huu wanapaswa
kujiepusha na kasumba za upinzani ambazo malalamiko kwao
  imekuwa ni sehemu ya sera inayopaswa kuachwa na wananchi
  hao.

Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mama
Asha Suleiman Iddi alihimiza kwamba Kiongozi lazima awe
mfano wa maendeleo ya jamii badala ya kushabikia vurugu na
  siasa chafu.

Mama Asha alisema siasa ni kwa Viongozi kusimamia juhudi na
  harakati za kiuchumi na maendeleo za wale wanaowaongoza kwa
lengo la kuwakomboa kimaisha.

Akitoa Taarifa fupi ya uanzishwaji wa vikundi hivyo vya
kiuchumi Afisa Mtendaji wa Kata ya Kilagano Bibi Pulkena
Malekela alisema jumla ya vikundi 71 vimeanzishwa katika
kata hiyo ili akinamama viwasaidie katika kujikwamua
kiuchumi.

  Bibi Pulkena alisema kati ya vikundi hivyo 26 viko tayari
kut oa huduma vikipata msaada wa uwezeshaji kutoka Mbunge wa
  Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama.

Hata hivyo Afisa Mtendaji huyo wa Kata ya Kilagano alielezea
changamoto zinazovikabili vikundi hivyo  kwa hivi sasa
  akizitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji pamoja na
huduma za umeme.

Akitoa msalamu zake mbunge wa Jimbo la Parameho ambae ndie
 mwenyeji wa ziara hiyo Mh. Jenista Mhagama alisema Serikali
ya Chama cha Mapinduzi imefanya mengi katika kuwaletea
  maendeleo wananchi wake.

Mheshimiwa Jenista Mhagama alieleza kwamba kero nyingi
  zilizokuwa zikiwakabili wananchi katika sehemu mbali mbali
  hapa Nchini Mijini na Vijijini zimepungua hasa huduma za
maji safi, afya na elimu.

Katika kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
  alichangia Shilingi Milioni 1,500,000/- kusaidia Vikundi
  hivyo pamoja na kuahidi nguvu za uwezekaji kwa majengo ya
  vikundi hivyo.

Balozi Seif pia akachangia shilingi Milioni 1,500,000/-
kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Lugagala pamoja na
kuahidi kutoa mifuko mia tano ya saruji ya ujenzi wa kituo
hicho.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/10/2014.

No comments:

Post a Comment

Pages