Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Wananchi (CUF),
Mkoa wa Tabora kimepanga kufanya maandamano ya kumpokea Naibu Katibu Mkuu Mpya
wa Chama hicho Magdalena Sakaya wakati atakapowasili kwa mara ya kwanza mkoani
hapo baada ya kupata cheo hicho na kuwatetea wananchi wa eneo hilo wakiwemo
wakulima wa zao la Tumbaku
Akizungumza katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Lombe Kata ya Kumbiziganga
wilayani Kaliua mkoani Tabora Katibu wa Chama hicho ambnaye pia ni mjumbe wa
Baraza Kuu la Uongozi Taifa Kapasha Kapasha alisema Chama chao kimeweka
historia katika Taifa kwa kumpatia cheo hicho kuliko vyama vingine vyovyote vya
kisiasa hivyo watampokea kishujaa kwa kufanya maandamano akitokea wilayani
Kaliua baada ya kutembelea Kata zote za Wilaya hiyo.
Alisema Sakaya ni
mpiganaji wa kweli ambaye anatetea haki za wakulima wa Tumbaku na wale wananchi
wanaonyanyaswa katika na Serikali kwa madai kuwa wanandishi ndani ya hifadhi
wakati wao wenyewe wanajenga vituo vya polisi ndani ya maeneo hayo.
"Haijwahi kutokea kwa
Mwanamke kushika wadhifa kama huo alionao Sakaya hivyo kutokana na Chama
kumuamini tutampokea kwa maandamano makubwa ili kuonyesha kuwa CUF haina ubaguzi
wa watu bali inaangali uwezo wako wa kufanya kazi na kupambana na mafisadi
ambao hata wakulima wanazulumiwa naSerikali ipo"alisema Kapasha.
Kapasha alisema, Chama
cha Mapinduzi (CCM), kimeufanya Mkoa wa Tabora kuwa ndio sehemu yake ya kuvunia
kura katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika lakini ndio mkoa unaoongoza
kwa watu wake kuwa masikini wakati ndio wazalishaji wa Tumbaku, na baadhi ya
madini ambayo yanapatikana kati mkoa huo.
Kwa upande wake Naibu
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Abdul Kambaya alisema mama huyo
ni shujaa kwani aliwekwa mahabusu kwa siku 14 baada ya kujitokeza hadharani
kuwatetea wafugaji walichukuliwa ng'ombe zao na Serikali ya CCM
"CCM ndio wanatumia
umasikini wenu kujipataia kura za ushindi maana haiwezekani miaka 20 ya wabunge
wenu katika majimbo haya hakuna maji safi wala barabara ya lami wakati
wanamfuko wa jimbo na ukitaka kujijua kuwa wewe ni masikini angalia vitu
vitatu ambayo chakula unachokula, sehemu unayolala na na nguo unazovaa ukiona
unafanya vitu hivyo bila mapenzi yako ujue wewe ni masikini kwani unahitaji
kula nyama lakini unakula wali na maharage ujue wewe ni masikini kwani huna
uwezo wa kununua"alisema Kambaya
Alisema haiwezekani kwa
miaka 50 ya uhuru watoto waendelee kukaa chini wakati hii hii ni tajiri kuliko
nchi zote zinazoizunguka lakini ndio yenye umasikini wa kutisha lakini viongozi
wanaangalia familia zao na ndugu zao bila kujali wananchi waliowachagua.
Sakaya ambaye pia ni
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora anatarajia kumaliza ziara yake leo
mkoani Tabora kwa kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara kama Naibu Katibu Mkuu mpya
wa CUF Tanzania Bara baada ya kurithi nafasi hiyo kwa mtangulizi wake Julius
Mta.
No comments:
Post a Comment