NA Mwandishi Wetu
UMOJA wa
Wafanyabiashara Walemavu Dar es Salaam (UWAWADA), umesema baada ya Bunge
maalumu la Kutunga Katiba kumaliza kazi yake, kilichobaki sasa ni wananchi
kupatiwa elimu ya kutosha iliwafanye maamuzi sasa hihi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa UWAWADA, Mohamed Kidumke, alisema ni vema Watanzania sasa
wakaachwa waijadili Katiba hiyo inayopendekezwa ili waweze kujiua kilichomo ili
waipigie kura kwa uhakika.
Alisema,
elimu hiyo itawasaidia Watanzania kujua kama maoni yao waliyopendekeza wakati wa
Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Jaji Joseph Wariyoba yameingizwa
kwenye katiba hiyo iliyopendekezwa.
“Serikali
inabidi iongeze nguvu binafsi mpaka watu waelewe na kuweza kupiga kura, kwa sababu wananchi wengi kama hawaikubali kutokana
na kuona baadhi ya maoni yao ya muundo wa serikali tatu kuachwa na kurudishwa
serikali mbili hali inayowafanya wananchi kugawanyika, hivyo elimu ya kutosha
inahitajika,”alisema Mohamed.
Kidumke,
lishauri serikali pamoja na vyombo vya dola kutoa uhuru kwa kila mwenye uwezo
wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu katiba hiyo kwa sababu wengi bado hawajajua
kilichopendekezwa na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba,
Aliongeza
kuwa kama serikali itawanyima wananchi kujua kilichoandikwa kuana hatari wakaja
wakafanya maamuzi ya kubahatisha kitendo ambacho hakina maslahi kwa Taifa.
“Wananchi
tuachwe tufanye maamuzi wenyewe, wanasiasa, vyombo vya dola visituoingilie
pindi wanapokuja watu kutupatia elimu,”alisema Kidumke.
Akizungumzia
kuhusu maoni yao kuingizwa katika katiba inayopendekezwa, Kidumke, alisema kwa
kiasi kikubwa yameingizwa.
Alisema
mjumbe wao alifanyakazi kubwa ya kusimamia maoni yao, na wanampongeza kwani
alihusika katika kamati na hata kwenye uandikaji.
Kidumke,
alisema katiba hiyo imegusa karibu makundi yote kama vile Watu wenye ulemavu,
wakulima, wavuvi na wengine ambao baadhi ya taasisi zimesikika zikiipongeza.
Hata hivyo,
alisema mvutano unaojitokeza kati ya vyama vya siasa na wanaharakati ni kawaida
ya demokrasia, kwamba kila mtu anayo haki yakupendekeza anachotaka lakini
mwisho wa siku sio rahisi kila maoni ya mtu kuingia kwenye katiba hiyo.
No comments:
Post a Comment