Mhariri
Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya, akikabidhi cheti kwa mwanafunzi
Ahmed Adamu katika mahafali ya tano ya wahitimu wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti
wa walimu wa maarifa ya Uislamu Dar es Salaam, Suleiman
Gombe.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutambua wajibu kwa kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu kwa watoto wao.
Wito huo ulitolewa Dar es Salam na Mhariri Msanifu wa gazeti la MTANZANIA, Khamis Mkotya alipokuwa akizungumza katika mahafali ya tano ya Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.
Mkotya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo alisema ni lazima jamii ikubali kuondokana na kulalamika na badala yake iandae mazingira mazuri ya watoto wao kuhakikisha wanasoma kwa bidii.
“Bado siku chache wanafunzi wa kidato cha nne nchini, mtafanya mitihani ya kuhitimu lakini tambueni kumaliza elimu hii kwa ngazi yetu ni chachu ya kutafuta zaidi ya elimu.
“Na mkiwa hamtafanya hivi mtakuwa mmekwenda ninyume na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) ambaye amatutaka tutafute elimu hadi uchina. Na hata leo ukimaliza mtihani wa kidato cha nne na kuona umemaliza tambueni elimu mlionayo sasa ni sawa na elimu ya msingi,” alisema Mkotya.
Alisema ili maendeleo chanya yaweze kupatikana nchini ni lazima jamii ijiandae vema kuyapokea kwa kuwa na mkakati hasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii kwenye masomo yao.
No comments:
Post a Comment