BAADHI ya wafanyabiashara wilayani Ilala jijini
Dar es Salaam wamemuomba Mkuu wa Mkoa huo Said Meck Sadik (pichani) kuchunguza kama
utaratibu wa faini wanazotozwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi zinazingatia
sheria.
Wakizungumza kwaa nyakati tofauti jijini wafanyabiashara hao, wa maduka ya simu, vitafunwa na
Wamachinga, walisema kuna viashiria kuwa wamegeuzwa na kuwa mtaji wa polisi
hao.
Mmoja wa Wafanyabiashara aliyejitambulisha kwa
jina moja la Makwambe ambaye anaduka la simu Kariakoo, alisema wanamuomba mkuu
huyo wa mkoa afanye hivyo kwasababu faini zinazotozwa zimekuwa za majadiliano
zaidi bila ya kuwa na kiwango maalumu kinachotambulika kisheria.
“Kwa mfano sisi wenye maduka ya simu tukikamatwa
tunatakiwa kutoa faini sh 150,000 hata hivyo, tunapinga, na tunawataka watufikishe
mahakamani, baadala yakuazisha majadiliano ili kila mmoja wetu atowe kiasi chochote
ambacho tunamini hakiendi serikalini,”alisema Makwambe.
Makwambe, alidai kuwa hata sitakabadhi zenyewe
zinazotolewa wanazitilia shaka kama kweli ni halali, kwani hazigongwi mhuri wa
serikali.
James John, alisema alikamtwa juzi Jumapili akiwa
anafanya biashara ya kutembeza nguo ambapo alitakiwa kulipa faini sh 50,000
lakini cha kushangaza baada ya kushindwa kulipa aliambiwa atowe 25,000 ambayo
aliwapa na kupewa stakabadhi ambayo haikugongwa mhuri.
“Wale polisi hawako tayari kukupeleka Mahakamani
bali wanachotaka ni hela na ndio maana wakitukamata wanatuambia mwenye sh
10,000, 15,000 au 20,000 haya unganisheneni fasta kiukweli wanakusanya hela
nyingi kwasababu wanaokamatwa kila siku hawapungui 300, fika pale mwenyewe utajionea kwani ule ni mradi wa wajanja ,”alisema.
John, alisema inapotokea kama kuna walioshindwa
kutoa kiwango chochote walichotakiwa inapofika wakati wa kuingia giza
wanaachiwa bila ya kufikishwa mahakamani, wakionywa na polisi hao kuwa
wasirudie tena baadala ya kuwapeleka mahakamani.
Fatime Alwaye, alisema polisi hao hawako tayari
kuwafikisha mahakamani kwa sababu mara nyingi wanapofika kule hawana ushahidi
baada kuviuza ama kuvila vitafunwa vyao.
Alisema kutokana na mazingira hayo, wanaona ni
bora wamalizane kwa njia hizo za kuchukuwa fedha kidogo ili wamuachie mhusika.
Fatime, alisema wanapinga utaratibu huo, na
kwamba wakibainika wana makosa basi wafikishwe mahakamani ambako wanaamini haki
itapatikana ikiwa ni pamoja na kurudishiwa bidhaa zao.
“Hivi sasa wakitukamata hawataki kuorodhesha
mali zetu wanaondoka nazo pamoja na vitendea kazi ambayo tumetumia gharama
kubwa kuvinunua, tunaomba tuwe tunarudishiwa vitu vyetu sio wakaviuze bila
kufuata sheria,”alisema Fatime
Aidha, Fatuma, aliahidi kuwa leo atampelekea mwandishi
sitakabadhi ambazo anadai kuwa si za serikali bali za kifisadi.
No comments:
Post a Comment