Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akifurahia kazi za amali zinazofanywa na
akina Mama wa Vikundi vya Ushirika vya Jimbo la Magomeni na kushawishika
kununua mkeka wa asili ya Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania {
UWT } Jimbo la Magomeni wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Mke wa Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani akilifungua
Baraza hilo.
Mama Asha Suleiman Iddi akilifungua Baraza Kuu la UWT Jimbo la
Magomeni kwe3nye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Tawi la Nyerere Mjini Zanzibar. (Picha na
Hassan Issa wa OMPR – ZNZ).
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Akinamama nchini wana wajibu wa kujiepusha na makundi ambayo ndio adui mkubwa katika harakati za maendeleo na Kisiasa hasa
wakati huu wa Taifa likikaribia kuelekea katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka
2015.
Mke wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo wakati
akilifungua Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jimbo la Magomeni linalofanyika
katika ukumbi wa Ofisi ya Tawi la CCM Nyerere Wilaya ya Mjini Zanzibar.
Mama Asha
alisema njia pekee ya kufikia maendeleo hayo ni kwa akina mama hao pamoja na
wananchi wote kufanya kazi zao kwa bidii na maarifa ili kufikia malengo
wanayojipangia kuyatekeleza.
Alisema
kamwe hakutakuwa na miujiza itakayoletwa na baadhi ya watu kwa kutaka
kufanikisha maslahi yao binafsi kupitia udanganyifu wanauelekeza kwa wananchi hasa wanawake ili kufikia azma yao.
Mama Asha
alifahamisha kwamba CCM ndio chama pekee Nchini Tanzania chenye uwezo wa
kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na sera zake zenye uwezo wa kutekelezeka
wakati wote.
Aliwatahadharisha
akina mama hao kuwa na tahadhari na watu
waliowahi kuneemeka na Serikali zilizopo madarakani ambao wakati huu wamekuwa
wakizipinga kwa vile wako nje ya utumishi.
Alieleza
kwamba ushawishi wa watu hao ulifikia hatua ya kuwataka watu wawe vilema kwa
sababu tu ya uchu wao wa madaraka ya nchi hii bila ya kujali kuwa vitendo vyao
hivyo vina muekeo wa kujenga chuki za maisha ndani ya jamii.
Katika
kuunga mkono vikundi vya kiuchumi na ushirika vya akina mama hao wa Jimbo la
Magomeni Mama Asha alisema kupitia Umoja wao wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge
wa CCM Zanzibar wataangalia uwezekano wa kusaidia akina mama hao.
Aliuomba
uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania { UWT } Jimbo la Magomeni kuviorodhesha
vikundi hivyo pamoja na muongozo wa shughuli wanazozifanya akina mama hao ili
vipatiwe msaada unastahiki kutokana na kazi zao.
Mapema
akitoa taarifa fupi ya Umoja wa Wanawake Tanzania Jimbo la Magomeni Katibu wa
UWT Jimbo hilo Bibi Maimuna Bara bara alisema akina mama wa Jimbo hilo wako
imara kuisubiri Katiba iliyopendekezwa na Bunge la Katiba kwa ajili ya kuipigia
kura ya ndio wakati ukiwadia.
Bibi Maimuna
alisema akina Mama hao wamewapongeza Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa
uwamuzi wao wa kupendekeza Katiba inayotoa fursa sawa ya hamsini kwa hamsini
kijinsia kwenye nafasi za uongozi pamoja na maamuzi ya Taifa.
Alisema
katika kukabiliana na ukali wa kimaisha akina mama wa Jimbo hilo tayari
wameshaanzisha vikundi 11 vya kuweka na kukopa sambamba pia na kuanzisha vikundi
vya vikoba.
Hata hivyo
Bibi Maimuna alieleza kwamba zipo changa moto zilizojitokeza katika vikundi vyao
akizitaja kuwa ni pamoja na ufinyu wa elimu kwa wana vikundi, vitendea kazi
kama Kompyuta pamoja na ukosefu wa fedha za kuendeshea miradi yao.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/10/2014.
No comments:
Post a Comment