Kikosi cha Kampuni ya TTCL mpira wa miguu kilichoshiriki Bonanza la Shirikisho la Michezo la mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) jana viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha UDSM mpira wa miguu kilichoshiriki Bonanza la Shirikisho la Michezo la mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) jana viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha TBc1
Kikosi cha TBc1
Mshambuliaji wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Francis Peter akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Kampuni ya TTCL, Addo Mgombelwa wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonanza la Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililofanyika
kwenye viwanja vya Chuo Kikuu (UDSM) jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Francis Peter akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Kampuni ya TTCL, Addo Mgombelwa wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Bonanza la Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililofanyika
kwenye viwanja vya Chuo Kikuu (UDSM) jijini Dar es Salaam.
Mpambano kati ya timu za Mpira wa Miguu za TTCL (wenye jezi za njano) na TANESCO wenye kijani kwenye Bonanza la SHIMMUTA.
Mpambano kati ya timu za Mpira wa Miguu za TTCL (wenye jezi za njano) na TANESCO wenye kijani.
Mpambano wa mpira wa pete ukiendelea katika Bonanza la Shirikisho la Michezo la mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililofanyika viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Safini Kajegule kutoka kampuni ya TTCL akimalizia mbio za magunia katika Bonanza la SHIMMUTA.
Timu za kuvuta kamba katika Bonanza la SHIMMUTA kwenye viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam zikipambana.
Timu za kuvuta kamba katika Bonanza la SHIMMUTA lililofanyika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam zikipambana.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
OFISA
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura
Oktoba 11, 2014 amezinduwa Bonanza la Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililofanyika
viwanja vya Chuo Kikuu (UDSM) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hotuba yake, iliyosomwa kwa niaba na Ofisa Mkuu wa Biashara wa
TTCL, Kanda ya Dar es Salaam, Karim Bablia aliwataka washiriki wa
bonanza kutumia nafasi hiyo ya kuwa pamoja ili kufahamiana zaidi,
kubadilishana mawazo na kushirikiana.
“…Bonanza
hili limetuwezesha sisi Wanamichezo Wafanyakazi kuweza kufahamiana
miongoni mwetu, kubadilishana mawazo ya nini kinafanyika kwenye kampuni,
mashirika au taasisi zetu ikiwa ni pamoja na kupeana taarifa za huduma
na bidhaa tunazotoa kwa wateja wetu na wananchi kwa ujumla,” alisema Dk.
Kazaura.
Aidha aliipongeza Kamati ya
maandalizi ya bonanza hilo kwa kitendo cha kuwakutanisha pamoja
wanamichezo hao, kwani mbali na kushindana kimichezo na kufahamiana
wanapata fursa ya kujenga afya za wafanyakazi, umoja na undugu.
Alizishauri
taasisi hizo kutenge muda maalum wa kufanya mazoezi kwenye taasisi zao
kila siku kwa lengo la kuimarisha afya na kuiwezesha miili kuwa na nguvu
ili kuzalisha tija zaidi kwenye sehemu zao za kazi, kwani taasisi kuwa
na mfanyakazi lege lege haiwezi kuzalisha tija zaidi mahali pa kazi.
“…Napenda
nitumie nafasi hii kuwapongezeni Kamati nzima ya Utendaji ya SHIMMUTA
kwa jambo hili kubwa mlilofanya ambalo kusema kweli limetukutanisha sisi
wanamichezo wafanyakazi mahala pamoja na kuweza kufanya michezo
mbalimbali ambayo kwa hakika, naona imewawezesha
Wanamichezo Wafanyakazi wa rika zote kucheza kila mmoja na mchezo aliouzoea.
Hata
hivyo alizipongeza taasisi na mashirika yaliyoshiriki katika bonanza
hilo ikiwemo kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Chuo cha Tiba
Muhimbili,(MUHAS) Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Taasisi ya Mifupa (MOI) Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania (OUT).
Taasisi nyingine
zilizoshiriki bonanza hilo ni pamoja na Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
Pamoja
na hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu huyo wa Kampuni ya TTCL aliishauri
SHIMMUTA kufikiria kuanzisha mabonanza kama hayo mikoa mingine ili
kuhamasisha michezo kwenye mikoa hiyo na kujenga mahusiano mema miongoni
mwa Wafanyakazi wa nchi hii. Mashindano yenyewe ya SHIMMUTA kwa mwaka
2014 yanatarajia kufanyika Mkoa wa Tanga kuanzia Novemba 20, 2014,
ambapo itashirikisha michezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment