Na Bryceson Mathias, Chalinze
MWENYEKITI wa CHADEMA Korogwe, Mjumbe wa Baraza Kuu na na
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Aulelian Nziku, amempongeza na kumkaribisha
Chadema Mkuu wa Wilaya, Mrisho Gambo, ashiriki kukomesha Rushwa na Ufisadi
nchini, huku akidai amekumbuka Shuka Asubuhi.
Akizungumza wakati anarudi toka kwenye kikao cha watia nia ya Ubunge Chadema Dar
es salaam, Nziku alisema anampongeza Gambo kwa sababu amefanyia kazi Kelele za
Chadema Majukwani, ambapo kelele hizo zilimfikisha Tume ya Maadili ya Umma
kuhojiwa.
Nziku alisema, Sababu za Gambo kupongezwa na Chadema Korogwe
zinatokana na hivi karibuni kutakiwa kukamatwa afikishwe kwenye Baraza hilo kwa
kile kinachodaiwa na wananchi aliwatia Lupango Wenyeviti na Watendaji
waliotafuna fedha za Ujenzi wa Maabara.
Aliongeza kuwa, “CCM Gambo hakumfai, na aelewe Sababu za Wananchi
Korogwe kumpokea kwa Nderemo akitoka Baraza la Maadili walikomtosa wana CCM
wenzake, kunatokana na kufanyia kazi Kauli za Chadema Majukwani, kuhusu umizigo
wa watendaji na wenyeviti hao.
“Chadema tuliahidi na tutafanya; Kutawataja hadharni Watendaji,
Wenyeviti, Madiwani, Wabunge, na Wakurugenzi Mizigo katika Wilaya yetu,
wanaokwamisha Maendeleo ya Wilaya kwa Dhuluma, Rushwa, Ufisadi na kutafuna
fedha ya ‘Umma Hovyo hovyo’”.alisema Nzilu
Alisema, ukiona Panya anamtunishia Paka Misuli, Ujue Shimo la
kukimbilia lipo karibu; hivyo wana CCM kama Gambo, wanaofanya kazi ya kuwatetea
wananchi wanaodhulumiwa haki zao na Wenyeviti na Watendaji, wasiogope
wanapotishwa; Wabwatuke, Kimbilio lao ni Chadema tuunganishe Nguvu’.
Aidha alisema, anategemea kuwaanika Viongozi, Mgambo, Wenyeviti na
Watendaji wa Kijiji cha Kwamkole, Kata ya Kizara, Tarafa ya Magoma, waliomfunga
Kamba Mwananchi kwenye Mti, eti sababu hakutoa fedha za Maabara, wakiwa na
risiti Feki. “Huu si Unyama ule wa Ujangili”.alihoji Nziku.
No comments:
Post a Comment