Na Mwandishi Wetu
Maafisa habari mbalimbali
kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB
Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa
kutoa taarifa kwa wananchi.
Kongamano hilo linafuatia
matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku
ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata
Taarifa.
Miongoni mwa taasisi
zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na
Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini,
Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya
Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha
ya kupata mwaliko.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa
Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti akizungumza jambo wakati akifungua
kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National
Organization of Legal Assistance-nola) Bwana James Malenga akisisitiza
jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari
wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.
Afisa Habari na Utafiti wa Misa-Tanzania Bw. Sengiyumva
Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwenye mada aliyokuwa anaiwasilisha kwenye
kongamano la maafisa habari wa taasisi za kiserikali(hawapo picha)
Mfanyakazi wa Misa-TanzaniaBwana Idrisa Abdallah akizungumzia adha
anazozipata anapokuwa anakwenda taasisi na idara mbalimbali za serikali
kupeleka barua ama maombi ya taarifa.
Afisa habari wa Mahakama Bi. Mary C. Gwera akizungumza jinsi ofisi
yake ilivyopokea Tuzo ya Kufuli na ambavyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika
kutoa taarifa kwa umma.
Afisa Mwandamizi wa habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Bwana Abraham
Nyantori akielezea changamoto za utoaji taarifa katika taasisi na idara za
serikali.
Maafisa habari wakifuatilia kwa umakini mada ya Umuhimu wa Kutoa/Kupata
Taarifa serikalini kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea Bwana James Marenga.
No comments:
Post a Comment