Meneja wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za
kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa
shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo Mkoani Simiyu.
Mkuu wa wilaya ya Bariad
Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu
vya masomi ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na
kampuni ya Airtel Tanzania
Na Mwandishi Wetu
Msaada
huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya
fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma
masomo hayo shuleni hapo.
Akipokea
msaada huo mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amesema shule
nyingi wilayani hamo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa
vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa
masomo hayo.
“Ni
kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi
kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Bariadi hali
inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema
Bwana Sima.
“uhaba
wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya
sayansi ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi
wetu hapa Bariadi” aliongeza Bwana Sima.
Aidha
Bw. Sima ameishukuru kampuni ya simu ya airtel kwa kuona umuhimu wa
kuboresha masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo hali
ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
“Msaada
huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi
hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii
na hasa vitabu vya sayansi” alimalizia Bwana Sima.
Kwa
upande wake mkuu wa shule ya sekonderi Bariadi Bw. Pawa Lutema
akipokea vitabu hivyo, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utatuzi wa
changamoto ya vitabu vya sayansi na kisha kuahidi kuvitunza ili viwe
msaada kwa wanafunzi watakaosoma shuleni hapo.
Awali
meneja wa Airtel Mkoani Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada
huo wa vitabu amesema kuwa kampuni yake inaendelea na mpango wake wa
kutoa msaada wa vitabu kwenye shule mbalimbali nchini kwa lengo la
kusaidia ukuaji wa elimu nchini.
Msaada
huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia
utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo.
No comments:
Post a Comment