HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 20, 2014

KINANA ASHIRIKI KILIMO KATIKA SHAMBA LA WANANCHI KIJIJI CHA MKOTOKUYANA NACHINGWEA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe wakati alipowasili katika kijiji cha Nkotokuyana jimbo la Nachingwea katika mwendelezo wa ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara itakayomchukua siku 16 akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na srikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi katika vijiji mbalimbali , Majimbo na wilaya Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NACHINGWEA-LINDI) 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliiza Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya kufika kwenye shamba la ufuta alilolikagua leo kijijini hapo, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi 5 
Baadhi ya akina mama wanakikundi hichi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM huku wakiwa wameshika majembe yao. 6 
Kilimo kimepamba moto 16 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la wananchi la kijiji cha Mkotokuyana wilayani Nachingwea leo.

No comments:

Post a Comment

Pages