Waliokuwa viongozi wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga kupitia
CCM, wakionyesha kadi zao kabla ya kuzikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipojiunga na chama hicho
wakati wa mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijiji hapo juzi.
(Picha zote na Joseph Senga)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili
katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa
hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar),
Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma,
katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
Akinamama wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakicheza ngoma ya
asili, wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), baada ya kuwasili kijijini hapo, ambako
alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa
serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini,
wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa
Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika
mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Taifa la Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Julius Mwita (kushoto), akimkabidhi kadi ya
chama hicho, Mwenyekiti wa Kijiji cha Udomo Kata ya Uchama Jimbo na Wilaya ya
Bukene mkoani Tabora, Julius Lubala, baada ya kurudisha kadi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment