HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2014

OPARESHENI DELETE CCM YAVUNA WANACHAMA 350 MKOANI SINGIDA

Wananchi wapatao 350 waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida wakiwa wameshika kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku wakila kiapo cha uzalendo baada ya kujiunga na chama hicho kwenye moja ya mikutano ya 'Operesheni Delete CCM' uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,  Zanzibar, Salum Mwalimu, mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu akiwalisha kiapo cha uzalendo wanachama wapya katika Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi, katika moja ya mikutano 'Operesheni Delete CCM', uliofanyika mwishoni mwa wiki kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment

Pages