Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya
nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) wa www.tff.or.tz
ambapo jezi hizo zimewekwa.
TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya
Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani,
jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya
kupigiwa kura.
Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura
anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya
hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.
Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi
ya timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment