Na Mwandishi wetu
TIMU ya Coastal Union imesema kuwa umuhimu wa timu hiyo kufanya vizuri kwenye mechi yao na Polisi Morogoro itakayochezwa wikiendi ijayo ni mkubwa kutokana na kuimarishwa kwa safu mbalimbali kwenye kikosi hicho.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, James Nandwa aliyasema
hayo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika mechi ya kirafiki kati yao na
Mombasa Kombaini iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani na kumalizika kwa
timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Kwenye
mechi hiyo,Coastal Union ndio ilikuwa ya kwanza kuweza kupata bao lao kupitia
Rama Salum dakika ya 5 lililotokana na penati baada ya mshambuaji wa Coastal
Union,Behewa Sembwana kuangushwa eneo la hatari na Omari Sharifu wa Mombasa
Kombaini na mwamuzi wa mechi hiyo Isihaka Shirikisho kuamuru ipigwe penati
hiyo.
Bao hilo
lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza
kwa kasi kwa timu zote kushambulia kwa zamu na kuonyesha kandanda nzuri na la
kuvutia.
Wakionekana
kucheza kwa umakini mkubwa baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji
wao, Coastal Union waliweza kuendeleza wimbi la mashambulizi langoni mwa
Mombasa Kombaini huku wachezaji wake wakikosa kosa mabao ya wazi kwa kupiga
mashuti yaliyokuwa yakigonga mwamba na kurudi uwanjani.
Kutokana
na shambulio hilo,Mombasa Kombaini nao waliweza kujipanga vilivyo na kuanza
kucheza kwa umakini hali iliyowasaidia kufanikiwa kuandika bao la kusawadhisha
kwenye dakika ya 47 kwa njia ya penati kupitia Khalid Jumaa dakika ya 47
lililotokana na Nahodha wa Coastal Union,Mbwana Kibacha kuunawa mpira eneo la
hatari.
Alisema
kuwa kikubwa zaidia anachojivunia ni kuwa na kikosi kizuri na tayari
alishaelewa nini cha kufanya ili kuweza kupata mafanikio kila mchezo ambao
wanakabiliana nayo kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Timu yetu ni nzuri hivyo anachokifanya ni
kuhakikisha wachezaji wanajitambua kwa dhamira ya kufanya makubwa kwenye mechi
zao za Ligi kuu soka Tanzania bara hapa nchini “Alisema Kocha Nandwa.
Alisema
kuwa mchezo huo ni kipimo tosha kwa timu hiyo kabla ya kuwavaa maafande wa
Polisi Morogoro ikiwa ni muendelezo wa michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara
hapa nchini.



No comments:
Post a Comment