Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikabidhi dawa kwa mganga mkuu wa hospitali ya jimbo
la Mpendae Dr. Omar Shaban Amran wakati alipokabidhi sehemu ya madawa
kwa hospitali hiyo ambayo yametolewa na mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.
Salum Turki kiasi cha makontena ya dawa manne yenye thamani ya shilingi
Bilioni Moja na pointi Nne yatakayosaidia katika hospitali zote za
Zanzibar, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi amemalizia ziara yake leo katika mkoa wa Mjini Magharibi wilaya
ya Amani jimbo la Mpendae kabla ya kuendelea na ziara mikoa mingine ya
Zanzibar. (Picha na Fullshangwe)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya ukarabati wa barabara kwa
kusambaza kifusi katika barabara inayounganisha hospitali ya Jimbo la
Mpendae na Barabara kuu ya Mchina.
Umati wa watu waliohudhuria ukifuatilia mambo muhimu yaliyokuwa yakielezwa na Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani.


No comments:
Post a Comment