Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro
Nyalandu (kushoto) katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara
ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli (kushoto) akikaribishwa na
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil
jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter
Msigwa (kushoto) akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya
Saudia Dk. Abdulrahman Al-Zamil jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tano kushoto) ukiwa
katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudia Dk.
Abdulrahman Al- Zamil (wa sita kushoto) mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo baina ya pande mbili jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine
pichani kutoka kushoto ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori Herman
Keraryo; Mkurugenzi Mkuu TANAPA Allan Kijazi; Mhe James Lembeli; Mhe Peter
Msigwa; Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru pamoja na
maafisa kutoka Chemba ya Biashara ya Saudia.
No comments:
Post a Comment