Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa jiji la Mwanza na Kanda
ya Ziwa wameiomba Kampuni ya Msama
Promotions inayoandaa Tamasha la Pasaka na Krismasi kuwapa
nafasi ya upendeleo kwa kuwapelekea
tamasha katika mkoa huo.
Sababu za kupewa kipaumbele
katika Tamasha la Pasaka mwaka huu ni baada ya kulikosa Tamasha la Kirismasi
ambalo lilifanyika kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa na
Songea.
Kwa mujibu wa
wakazi hao ambao waliwaomba waandaaji wa
matamasha hayo ya injili, Kassim Mtolea mwanafunzi wa
Chuo cha SAUT wanamuomba Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Alex
Msama na kamati yake kuwafikiria kwa sababu linashirikisha waimbaji wa Kimataifa.
Mtolea alisema wanamuomba
Msama kuwafikiria zaidi
kwa sababu miaka
yote tangu limeasisiwa limekuwa likianzia jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema waandaaji
wakabadilika na kulipeleka kwanza Jijini Mwanza.
Aniceth Nyahore
ambaye ni mkazi
wa Maswa lalieleza kuwa iwapo tamasha hilo litaanzia Mwanza litakutanisha
mikoa ya Geita,
Shinyanga, Mara na
Kagera katika uwanja wa CCM Kirumba na kueneza injili pamoja na burudani.
Nyahore alisema
ubora wa Matamasha
hayo unatokana na ushiriki wa waimbaji wa Kimataifa wanaotoka
nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda,
Rwanda na Uingereza ambao umekuwa ukivutia umati mkubwa
wa mashabiki.
Daniel Mkate
aliishauri Kamati ya maandalizi kuzingatia kuanza na mkoa wa Mwanza baada ya kulikosa Tamasha la Krismasi
lililofanyika mwaka jana huku wakazi hao wakiwa na kiu kubwa.
Sambamba na
kuliomba tamasha hilo
mkoani humo pia
aliishukuru Kamati ya
Maandalizi kwa kumleta
muimbaji Rebecca Malope ambaye alishiriki tamasha la mwaka
juzi.
Aidha Mwenyekiti wa maandalizi
ya tamasha hilo, Alex Msama alikiri kupokea maombi haya ambapo alisema ni
vigumu kutoa maamuzi maana bado ni mapema mno, lakini aliahidi kuyafanyia kazi.


No comments:
Post a Comment