HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2015

MGOGORO ULIOZUIA MRADI WA MAJI LUGULUNI WAPATA SULUHU

MGOGORO uliyokwamisha mradi mkubwa wa maji katika vitongoji vya Liwale na Kwamsamati, vilivyoko mtaa wa Luguluni Kata ya Kwembe wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam sasa umepatiwa suluhu.
Mradi huo, unagharimiwa na Kampuni ya Majitaka na Majisafi, Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, huku wananchi wakichangia kidogo kumalizia mita 200 hadi 450 zilizobaki kufika katika vitongoji hivyo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika juzi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdulhaman Said, alisema kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kulitokana na mradi huo kuwa na kamati tatu ambazo zimezua maswali kwa wanachi.
Suluhu ya mgogoro huo ilipatikana juzi baada ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo kukubaliana na wananchi kuchagua wajumbe wanane wa Kamati ya Maji ya vitongoji hivyo ambapo kila upande wa utatoka wajumbe wanne.
Wajumbe hao ni Shamne Liperatusi Elizabeth Isihaka, Vicent Makundo na Mogosi Shingilila hawa ni kutoka mtaa wa Liwale.
Wengine kutoka Kwamsamati ni Shomari Diwaga, Hippy Kihiyo, Coletha Paul na Edgar Jave.
“Hatukuja hapa kuvunja kamati yenu iliyokuwepo awali bali tumekuja hapa kuchagua kamati moja ambayo itakuwa na baraka zote  za wananchi,”alisema Said.
Said, alisema serikali ya mtaa huo iliamua kufanya hivyo ili kuondoa aibu kwamba viongozi wa mtaa huo ndio wanaokwamisha mradi huo huku wananchi wakiteseka.
Aidha, baada ya kumilika kazi ya kuchagua Kamati hiyo, wanatarajia kuanzia jana wangekamilisha utiaji saini wa barua na muktasari iliyokuwa ipelekwe Dawasco kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ili wananchi waanze kupata maji.
Ofisa Mtendaji, Ramadhan Kanuwa, aliwataka wajumbe wa Kamati hiyo kujipanga haraka ili waweze kwenda kufungua Akaunt Benki jambo ambalo ni muhimu mno kwa jumuiya ya watumia maji.

No comments:

Post a Comment

Pages