HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2015

MSAMA ALIPIA ADA YATIMA DAR

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo ikiwemo kulipia ada wanafunzi Yatima wa vituo vitano vya Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya tamasha hilo, Khamis Pembe. (Picha na Francis Dande) 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya tamasha hilo, Khamis Pembe.
 Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. 


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewalipia ada ya masomo wanafunzi yatima wa vituo vitano vya jijini Dar es Salaam waliokuwa wamesimama masomo kuwawezesha kuendelea na safari yao ya elimu kwa maslahi yao na taifa.
Akizungumza leo Ofisini kwake Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama alisema japo ni utaratibu wao wa kusaidia makundi maalumu katika jamii tangu mwaka 2000, safari hii wamepanga kuongeza idadi ya vituo vitakavyopatiwa msaada wa ada.
Alisema kwa kutambua umuhinmu wa elimu kama mwanga na msingi wa maisha, Kamati yake imeamua kusaidia eneo hilo kwa kuwalipia ada watoto yatima wa vituo vipatavyo 25 katika mikoa mbalimbali, vikiwemo vitano vya jijini Dar es Salaam.
Msama amevitaja vituo ambavyo wanafunzi wake waliokuwa na tatizo la ada na tayari wamewalipia ni Malaika Kids, Mwandaliwa, Honoratha, Maunga Centre na Istikama kwa lengo la kuwezesha wanafunzi hao kupata elimu ambayo ni mwanga katika maisha yao ya baadaye.
Safari Kamati ya Tamasha la Pasaka imgeguswa zaidi na wanafunzi waliokosa ada hasa kutokana na kilio kilichotolewa  hivi karibuni na mwanafunzi wa kidato cha nne wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa ambaye alisimama masomo kwa tatizo hilo.
Alisema Jumanmosi iliyopita wakati akitoa misaada ya vitu mbalimbali katika vituo vya yatima kikiwemo cha Mwandaliwa, mwanafunzi huyo alitoa kilio chake wakati wa kutoa shukrani kwa misaada iliyokuwa wamepatiwa na kusema ikiwezekana asaidiwe ada ili arejee shuleni aweze kumaliza kidato cha nne.   
Alisema kutokana na uzito wa ombi hilo, Msama Promotions imeamua kufanyia kazi haraka ili wanafuzni hao warejee shuleni na kuongeza baada ya Dar es Salaam, watafanya hivyo pia katika mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma, Dodoma Shinyanga na Tabora.
Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua kuwa hilo moja ya malengo ya msingi ya Tamasha hilo katika kipindi hiki cha maandalizi ya Tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu litaadhimisha miaka yake 15 tangu lianzishwe mwaka 2000.
Aliongeza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Tamasha hilo hadi sasa ikiwa ni miaka 15, kiasi cha shilingi mil 17 kimetumika kusomesha watoto yatima huku misada kwa ajili ya wanawake wajane ikifikia shilingi mil 76 na kwamba kwa mwaka huu, wamepanga kutoa baiskeli 100 kwa wenye ulemavu katika mikoa mbalimbali.
Aidha, Msama amesisitiza kuwa jukumu la kulinda jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), liwe la jamii nzima katika kuhakikisha nao wanaishi kwa usalama na amani kwa vile nao wana haki ya kuishi kama wengine.
Alisema Kamati yake imepanga kutumia Tamasha la Pasaka la mwaka huu, kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili dhidi ya albino na kuisihi serikali kuongeza vita ya kuwasaka wahusika na kuchukuliwa hatua za kisheria pale wanapothibitika pasipo shaka.
Msama alirejea tena wito wake wa kuisihi serikali pia kuangalia uwezikano wa kujenga kituo maalum kwa ajili ya kuwalea watoto wenye ulemavu huo kwa ajili ya  usalama wao ambapo baada ya kuwa watu wazima, ndipo warejee mitaani wakati huo mapambano dhidi ya vitendo hivyo yakiongezwa kasi.

No comments:

Post a Comment

Pages