HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2015

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Takwimu za Uchumi, Morice Oyuke, amesema pato la Tifa katika robo kipndi cha robo ya tatu ya mwaka 2014 limeongezeka kwa kasi ya asilimia 6.8 ikilinanishwa na asilimia 7.4 mwaka 2013.

Akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Oyuke, alisema takwimu hizo zilizowasilishwa jana ni za Julai hadi Septemba, kwa bei za miaka inayohusika na mwaka wa 2007, ambazo zinasambazwa kwa mara ya kwanza.

“Hizi ni kwa kuzingatia marekebisho ya takwimupato za pato la taifa kwa bei za mwaka 2007,”alisema Oyuke.

Alisema, kupanda kwa takwimu hizo za pato la taifa kulitokana na ongezeko la ukuaji wa nishati ya umeme kulikotokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na mafuta na gesi.

Oyuke, alisema, takwimu hizo za pato la taifa hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu, mitatu ambavyo ni Januari hadi Machi, Aprili hadi Juni, Julai hadi Septemba na Oktoba  hadi Desemba.
“Utayarishaji wa takwimu za pato la taifa hujumuisha shughuli zote za kiuchumi na hivyo hutumika katika kutathimini, mipango na kutayarisha sera za kiuchumi,”alisema Oyuke.


Aidha, shughuli nyingine kama vile huduma za malazi na chakula zilikua kwa kasi ya 0.2 ikilinganishwa na asilimia hasi 0.4, shughuli za habari na mawasiliano nazo zilikuwa kwa asilimia 11.9 katika robo mwaka ya tatu 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment

Pages