HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 27, 2015

UTT YATOA SEMINA YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWENYE MASOKO YA FEDHA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA

Ofisa Masoko Mwandamizi kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya UTT, Martha Mashiku akitoa semina kuhusu uwekezaji wa pamoja kwenye Masoko ya fedha. Akizungumza na washiriki wa semina hiyo Mashiku alisema kuwa kazi kubwa inayofanya na UTT ni kuwawezesha watanzania wote wenye vipato tofauti kushiriki kwenye masoko ya fedha, kwa kujiwekea akiba taratibu huku pesa inawekezwa kwenye masoko ya fedha na mitaji. Ofisa huyo alisema UTT imekusudia kutoa elimu kwa makundi mbali mbali ya jamii ili watambue fursa hii ya kujiwekea akiba huku fedha zao zikikua kwa kiwango shindani kwenye soko.
Mwenyekiti wa Kikundi cha wanawake wajasiriamali wenye Ulemavu (Fuwavita), Mathayo Kawogo akitoa shukrani kwa kampuni ya UTT kwa kutoa mafunzo juu ya uwekezaji wa pamoja kwenye masoko ya fedha. Aliwasisitiza washiriki kutumia fursa zilizopo kujikwamua kwenye dimbwi la umasikini na hasa kutumia fursa ya UTT kuwekeza na ni huduma rahisi kujiunga na pia nafuu.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali wenye Ulemavu (Fuwavita), Mathayo Kawogo (kushoto) akikabidhi pesa taslimu kwa mlezi wa kikundi hicho, Mike Mwita, kwa ajili ya kuanza kuwekeza kwenye Mfuko wa Umoja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. 
Washiriki wa Semina ya Kuwajengea uwezo Wanawake Wajasiriamali wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina iliyoendeshwa na kampuni ya Uwekezaji ya UTT.

No comments:

Post a Comment

Pages