Spika wa Bunge, Anne Makinda (wa pili kulia) akiongozana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (wa pili kushoto) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume.
Spika wa Bunge, Anne Makinda (wa tatu kushoto) akikagua ujenzi wa nyumba za NSSF Mtoni Kijichi.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiangalia
ramani ya mchoro wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam, wakati
Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipotembelea kukagua miradi ya shirika hilo likiwemo Daraja la Kigamboni.
Wa pili kushoto ni Mhandisi wa NSSF, John Msemwa.
(Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo wakati Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipofanya ziara katika miradi ya shirika hilo, ikiwemo Daraja la Kigamboni, ujezi wa nyumba za bei nafuu zilizopo Mtoni Kijichi na mji wa kisasa wa Dege Eco Village.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akizungumza katika wakati wa majumuisho ya ziara hiyo. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na Mkurugenzi wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.
No comments:
Post a Comment