Naibu Kamishna
Upelelezi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Loicy Appolio, akiwa mbele ya
Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jana, ambapo anatuhumiwa kupokea mgawo wa
shs. milioni 80.85 kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering and
Marketing Limited, James Rugemalira. (Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Kamishna Upelelezi
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Loicy Appolio, leo amefuata nyao za
watangulizi wake watatu kupinga kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa
Umma na baadala yake amekimbilia Mahakama Kuu kuweka pingamizi.
Watangulizi hao watatu
waliokimbilia Maahakamani kupinga kuhojiwa kuhusu tuhuma za kupokea mgao wa fedha
toka Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, ni Mwanasheria Mkuu wa
zamani Endrew Change, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Nyumba ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rogonzibwa Mujunangoma na Mkurugenzi Mtendaji wa
Wakala wa Usajaili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Philip Saliboko.
Loicy, anatuhumiwa kupokea
mgawo wa sh.milioni 80.85 kutoka kwa mmiliki wa kampuni hiyo, James Rugemalira,
ni kinyume cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Pia analalamikiwa kuwa
hakutamka kwa kamishna wa maadili, Hotel anayoimiliki inayoitwa ‘Clasic Hotel
yenye thamani ya sh. milioni 150 iliyoko Kinondoni ambayo katika tamko lake la
rasilimali na madeni kwa kipindi kilichoishia Desemba 31, mwaka (2010, 2011,
2012, 2013 na mwaka 2014).
Wakili Ogunde aliwasilisha
pingamizi hilo baada ya Wakili wa Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Filotheus Manula kuwasilisha malalamiko hayo
dhidi ya Loicy mbele ya baraza hilo .
Wakili Ogunde aliwasilisha
pingamizi hilo
baada ya Loicy kukana malalamiko yote yaliyowasilishwa na Wakili Manula dhidi
yake.
Akiwasilisha
pingamizi hilo ,
Wakili Ogunde alidai baraza halina uwezo wa kusikiliza malalamiko dhidi ya
mteja wake kwa madai kwamba kuna amri ya
zuio iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa chombo chochote cha umma kushughulikia
suala lolote linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania
Limited (IPTL) pamoja linalohusu akaunti ya Tegeta Escrow.
Alidai zuio hilo lilitolewa kupitia
kesi ya msingi namba 5 ya mwaka 2014 iliyofunguliwa na IPTL na wenzake dhidi ya
Waziri Mkuu na wenzake saba na kwamba, baraza lina nakala ya amri hiyo.
Hatua iliyochukiliwa na
Loicy ni sawa na ile iliyochukuwa na mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge
na wenzake wawili, alipofikishwa mbele ya baraza hilo hivi karibuni.
Hata hivyo, Jaji Msumi,
alimweleza wakili Ogunde kuwa katika shauri dhidi ya Chenge, waliona baraza
lina uwezo wa kusikiliza kwa sababu baraza si sehemu ya waliopewa amri hiyo ya
zuio na Mahakama Kuu.
Kauli ya Jaji Msumi
ilijibiwa na Wakili Jamhuri, ambaye alidai amri ya zuio hilo
inavihusu vyombo vya umma na kwamba, baraza ni chombo cha umma, ambavyo
vimezuiwa kuendelea kushughulikia suala hilo
hadi kesi hiyo ya msingi iliyopo Mahakama Kuu itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Hoja hizo za Wakili Ogunde
zilipingwa na Wakili Manula huku akiomba muongozo kutoka kwa Jaji Msumi kwamba
mapingamizi hayo yatachukuwa muda gani
hivyo kuomba kesi hiyo iendelee.
Kabla ya Jaji Msumi kujibu
muongozo huo alimueleza Wakili wa serikali kuwa suala lililokuwa mbele yao lilkuwa tofauti na
yale yaliyotangulia kwani hili likuwa nalinahusu kesi mbili tofauti.
“Niombe kuwa wakati
mwingine mkajipanga katika fuata sheria kwa kuorodheshamashauri haya kwa namba
ambazo zitafafanua adhabu kwa kila makosa,”alieleza Jaji Msumi.
Jaji Msumi alieleza hivyo
baada ya kubaini katika tuhuma zilizowasilishwa
kulikuwa na suala lingine linalohusu Hoteli inayoitwa ‘Classic Hotel’
ambayo inathamani ya sh. milioni 150, ambalo nalo hili ni suala kubwa mno.
Akijibu muongozo uliyombwa
na wakili wa serikali kuhusu kikomo cha mapingamizi kwamba yatachukua muda
gani, elieleza kuwa itategemea wahusika kuharakisha mchakato wa kuwakirisha
rifaa zao katika Mahakama Kuu pia waelewe kuwa kuna muda wa kufanya hivyo na
wasijidanganye kama wanaweza kuchelewesha
muda.
No comments:
Post a Comment