HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 04, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI DODOMA NA KUANZA ZIARA WILAYA YA MPWAPWA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea mkoani Ruvuma ambako alihudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi Marehemu John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni, Chama cha Mapinduzi kilikuwa na maombolezo ya kitaifa ya siku tatu mpaka mazishi ya kiongozi huyo yalipofanyika jana yakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete.
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Ndugu Adam Kimbisa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Ndugu Mwigulu Nchema. 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanaCCM na wananchi waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. 5 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati alipokuwa akisalimia wananchi mjini Mpwapwa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Pages